Wewe ndio umechoka akili kweli! Hata daladala unayopanda tayari wengine wengi wameishaipanda. Gari kupandwa na wengine haikuzuii nawe kupanda. Wapi umesikia daladala imejaa? Acha uhuru wa watu uendelee kufaidiwa. Huyo mleta hoja hakusema ni original ya kwake bali imepatikana kwingineko, walioisoma unayoisema heri yao, lakini wengine hawakuiona na hii ni mara yao ya kwanza. Ungeweka mbadala wako sasa ajifunze huyo unayemkatisha tamaa. Zaleo karibu ukumbini, lete habari wala usikate tamaa. Ndivyo walivyo humu ndani, wanataka wasikilizwe wao tu watu fulani. Miaka 50 ya Tanganyika ikomeshe haya, tuachane kabisa na "Zidumu fikra za peke yake yuleyuleeeee!"