Whatsapp inatumia END TO END ENCRYPTION . Ili kuweza kutumia feature hii ni lazima wote mnaochati muwe mnatumia whatsapp latest version. Endapo mmoja wenu hana latest version, then hutopata feature hii.
End to end encryption inafanyaje kazi?
Unapoandika ujumbe ukiutuma unabadilishwa kuwa lugha isiyo eleweka (cipher text) na key ya kung'amua lugha hiyo inatumwa kwake yeye mpokeaji. Hivyo mpokeaji anapopokea ujumbe uliofungwa (cipher) key inliyotumika kuifunga ndio inayotumika kufungua ujumbe huo.
Mfano rahisi wa encryption.
Ujumbe ufuatao umefungw kwa funguo ya 1
Oblvqfoeb tbob.
Key =1
Tukiufungua ujumbe huu tunapata neno lifuatalo'
Nakupenda sana.