#What Balozi Sefue Should do

#What Balozi Sefue Should do

Sita Sita

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2008
Posts
1,449
Reaction score
622
Wakati huu ambapo Serikali inafanya mageuzi katika Fiscal Expenditure nadhani kuna masuala ambayo inabidi yafanyiwe maamuzi haraka ili kuinufaisha Serikali.

1. Harmonisation ya Mishahara ya Mashirika ya Umma. Kwa Mfano; it does not make sense kuona Afisa wa LAPF anapokea mshahara mkubwa kuliko wa PSPF wakati wanafanya majukumu yanayofanana. Hii ina maana Supporting Staff wa Mashirika ya Umma wanaofanya Accounting, Auditing, Procurement, HR Management etc. walipwe sawa bila kujali shirika linaingiza kiasi gani cha fedha.

2. Merging Pension Funds. Serikali inapoteza sana mapato kwa kuweka mifuko tofauti lakini inahudumia watu wale wale. PPF na NSSF should be merged and the same goes to LAPF PSPF na GEPF.

3. Watumishi wa Umma watumie Bima ya Afya ya Serikali NHIF. it doesn't make sense mtumishi wa umma anakatwa mshahara fedha zake zinaenda PSPF lakini Mtumishi huyo anatibiwa kwa bima ya NHIF lakini yule wa PSPF anatibiwa na bima ya AAR wakati huyu wa PSPF ni junior kuliko yule wa Wizara. Fedha za Serikali ziende kwenye Bima ya Serikali sio kunufaisha kampuni binafsi.

4. Ofisi za Serikali zilizo kwenye majengo ya Kampuni Binafsi au Watu Binafsi zihamishwe ziende kwenye majengo ya Serikali. Hili halina mjadala.

5. Mashirika ya Umma yawekewe targets za mapato na Msajili wa Hazina. Nashangaa TRA inajiwekea targets ndogo alaf kila siku wanajisifu wamevuka malengo. Hata mimi ningeruhusiwa ningejiwekea muda wa kuingia ofisini saa nne asubuhi alaf nikifika saa tatu nasema nimevuka malengo. If possible kuwe na formula au wawekewe target ya 130 percent kila mwaka hapo ndo watajituma zaidi.

6. Hakuna haja ya kuweka kampuni za Ulinzi ziwe zinalinda Maneno ya Serikali wakati kuna Jeshi la Polisi. Nashauri watumie Nusu ya hizi fedha kuwapa askari wa Jeshi la Polisi kama motisha. Mbona ATM zinalindwa na askari?! Hili linawezekana

7. Serikali itumie madereva kutoka JKT au Jeshi la Polisi maana madereva wengi tunaona wanaendesha magari ya umma vibaya na wanayaharibu. Ukiweka mtu mwenye nidhamu ya Jeshi anakua anaheshimu gari kuliko baadhi ya hawa madereva mnaotumia. Alaf hamna hajanya kutumia V8, RAV4 zinatosha.

8. Mashirika ya Umma yaanze kutoa ajira kwa mikataba. Hii itaongeza ufanisi wao na wataheshimu kazi. hii ianzie TPA TCCL TRL na ATC ambao wana watu lukuki ila wanachangia less than 1 percent ya bajeti ya Serikali.

9. Kuwe na Kipaumbele katika kununua huduma kutoka Mashirika ya Serikali. Ina maana mtumishi wa umma akipanda ndege lazima iwe ni ATC. Wanao stahili wanunuliwe mobile phones za TCCL ili wapewe airtime za TCCL sio kupeleka hela za Serikali Tigo na Fastjet.

10. Kuishi kwenye nyumba ya Serikali iwe ni kwa maximum of 2 terms each of 4 years. Haiwezekani mtu anakaa nyumba ya Serikali for 20 years lazima atajisahau kujenga. This should be applied kwa nyumba za NHC. unapewa contract ya 4 years ukimaliza una-renew only once. after that ondoka wapishe vijana waje kukaa.

Ruksa kuendeleza
 
ATC inafika MAREKANI,DUBAI,UINGEREZA N.K.!
 
ATC inafika MAREKANI,DUBAI,UINGEREZA N.K.!

Hiyo ban ya Foreign Trips umeielewa

Serikali inatakiwa kuthamini mali zake. sasa kama wao wenyewe hawataki kupanda ndege zao wanataka nani azipande. Kumbuka JPM kasema watumishi wa umma waende mikoani sio Marekani Dubai na Uingereza.
 
Naona unamikakati ya kuuwa sekta binafsi... Uchumi sio taaluma yako waachie wenye taaluma zao mkuu.. serikali ndio supporter mkuu wa sekta binafsi.. cha msingi hizo taasisi ziboreshe huduma zao kwenye soka la ushindani
 
Naona unamikakati ya kuuwa sekta binafsi... Uchumi sio taaluma yako waachie wenye taaluma zao mkuu.. serikali ndio supporter mkuu wa sekta binafsi.. cha msingi hizo taasisi ziboreshe huduma zao kwenye soka la ushindani

kaka sekta binafsi haiwezi kufa. kama ni uchumi nimebobea sana tu.
Sekta binafsi bado ina nafasi kubwa katika miradi ya maendeleo. ningesema Serikali iwe na kampuni za ujenzi kama China hapo ndo tungeua Private Sector ya Tanzania. Kumbuka Serikali inaibiwa sana na watoa huduma kwa kuweka bei danganyifu na mara nyingi wanaopewa hizo tender sio wale wanaostahili. huku ndio kunafanya sekta binafsi isikue kwa sababu hatuthamini wanaostahili kuthaminiwa.
 
Chuo Kikuu Dar ma Professor wamestaafu wapo kwa mikataba watakaa nyumba za Chuo. Vijana wapya Assistant Lecturers wanapanga mitaani.
Si ajabu wanapanga nyumba za ma Professor hao hao walioshikilia nyumba za Chuo.
 
Make some sense! One thing though .. improve your commercial and marketing perspectives!
 
Binafsi naona serikali ikiamua point namba 3, 5, 8, 9 na 10 zinaweza kutekelezwa ndani ya muda mfupi sana. Zilizobakia zina changamoto kadhaa hivyo zinahitaji muda zaidi mfano ofisi zote za serikali kuhamia kwenye nyumba za serikali pengine moja ya vikwazo inaweza kuwa uhaba wa hizo nyumba katika kukidhi mahitaji.
 
mkuu naunga mkono baadhi ya point, ila nipo kinyume na ww point namba 6&7 . Hizo point utasababisha ukosefu wa ajira kwa vijana waliopata mafuzo ya ulinzi vile vile na waliopata mafuzo ya udereva. watu wengi wasiokuwa na sifa za kufanya kazi officen wamepata ajira kwenya ulinzi na udereva.
 
ndugu ni TTCL na sio TCCL na mimi niongeze RAILWAYS NA KAMATA Buses zirudi wafanyakazi wa serikari wasafiri kwa warant
 
R.I.P. JPM

Naona uliweza kusoma akili yangu

Bado Na. 7, 8 na 10

I hope Mhe. Samia Suluhu Hassan atafanikisha
 
Back
Top Bottom