Khalidoun
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 2,834
- 4,463
Sophia Simba ni Mwenyekiti Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) tangu mwaka 2008.
Rais John Magufuli ni Mwenyekiti CCM tangu Julai 2016. Leo Magufuli ndiye mwenye chama, Sophia OUT. Sophia hana chake.
Siyo OUT kwa maana ya uongozi, yaani OUT kwamba CCM si yake tena. Haimhusu hata kidogo.
Nakumbuka Sophia aliwahi kuhamasisha wanawake kuwanyima unyumba waume zao ili kuwalazimisha waiunge mkono CCM aliyoipenda. Leo hii Sophia OUT.
Tamko la Sophia kuvuliwa uanachama limetolewa na Humphrey Polepole, kijana ambaye hana historia yoyote na CCM.
Emmanuel Nchimbi ni jina kubwa CCM. Bonge la mwanasiasa tangu mwenyekiti UVCCM, mjumbe Kamati Kuu. Leo anapewa onyo kali kupitia kinywa cha Polepole ambaye hana historia na CCM.
Edward Lowassa, mwanasiasa aliyekulia CCM tangu ikiitwa Tanu. Kigogo hasa. Chama kikamwamini mpaka akawa Waziri Mkuu. Leo yupo Chadema. Mwana-CCM akionekana na Lowassa anaonekana kirusi.
Frederic Sumaye, mmoja wa waliotafuna mema ya CCM. Uwaziri Mkuu miaka 10. Hakuna mwingine aliyekalia ofisi ya Waziri Mkuu muda mrefu kama yeye. Leo yupo Chadema. Haipendi tena CCM.
Kuna aliyeipenda Chadema kuliko Dr Willibrod Slaa? Alimwaga manyanga akiwa Katibu Mkuu. Aliumia, akasema na kusonya, leo hii yupo wapi? Yupo ughaibuni na maisha yanaendelea.
Zitto Kabwe ungempenda alivyojiamini alipokuwa Chadema. Akijenga hoja zake, akisimamia misimamo yake, leo hii yupo ACT-Wazalendo na maisha yanaendelea.
UJUMBE
Nani mwenye chama? Aliye na chama ni aliyeshika mpini katika wakati husika. Ambao hawajashika mpini wameshika tu makali, wakileta jeuri makali yanawafyeka.
Poleni wenye kufukuzwa na vyama, pia wenye kuondoka kwenye vyama bila kupenda.
Vyama vipo tu, ni njia tu. Ndiyo maana Lowassa aliona CCM hakuna njia akajiunga Chadema. Zitto aliona Chadema hakuna njia akajiunga ACT-Wazalendo.
Vyama ni njia ya kwenda wapi? Kwenda kupata madaraka na kujenga nchi. Ubishi wa vyama ni hoja kuhusu njia ipi bora kujenga nchi. Kwa hiyo, tusitoane roho kwa sababu ya njia, tutazame la muhimu ambalo ni ujenzi wa nchi.
Usisimamishe mishipa. Wapo waliosimamisha mishipa lakini walitemwa. Simamia nchi yako ndugu. Chama ni njia tu.
Ndimi Luqman MALOTO