Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,638
Umri unasogea unaamua kutafuta binti wa kuchumbia ili umuoe.Wakati ukitafuta mchumba kwa umakini Wachumba uliokutana nao wako hivi
1=Wa kwanza umekutana nae ukamposa akaonyesha kukubali haraka mkapeana namba za mawasiliano muendelee kuwa karibu.Jioni unashangaa anakutumia Meseji anakwambia "mume wangu hadi sasa sijala" unabaki kushangaa kuitwa mume ghafla hivyo kabla hata jujamtambulisha kwenu anataka umgharamie chakula wakati unaishi na wazazi wake.
2=Wa pili ulimposa mlipokutana ukamweleza nia yako akasema yupo tayari mkapeana mawasiliano.Ile mmeachana tu inaingia Meseji amekuandikia "yaani unaniacha hata kunipa elfu kumi nikasuke" moyo unakuambia hapa hakuna mke.
3=Wa tatu mmekutana kwenye sherehe ukampenda ukampa malengo yako juu yake akakuitikia vizuri.ukamwambia tukimaliza sherehe tukae kidogo tuongee akakubali.Ile unaondoka pale alipo anakuambia niachie hata bia nne basi hapa nisiboreke sana unapigwa na mshangao unamuuliza nikununulie bia gani anakuambia nakunywa Savanna na wewe mfukoni una huku 3 tu ya nauli.
4=Huyu wa nne umempendea ucheshi na upole ukamposa akakuzungusha baadae akakubali.mkaanza ukaribu wenu. Siku ya tatu anakupigia simu anakuomba umnunulie lasta na lotion ukajipapasa ukamnunulia ili usimkose.Ukampelekea na ile unaagana nae anakwambia mbona hujaniachia ya kusukia?unamuuliza ni bei gani anakwambia niachie 15,000/= inatosha ukijicheki hata buku tano huna unamwahidi kumtumia kwenye simu mnaagana kisha unablok namba yake.
5=Unampata mwingine ni mcha Mungu,mstaarabu,mzuri,mchapa kazi,hana tamaa,mnaongea anakuelewa,anakusindikiza hadi sehemu ya kupanda usafiri.unasimamisha daladala anakwambia mpendwa usipande daladala utasumbuka anatoa yeye elfu 5 anakwambia upande taxi.Unapokea baada ya kukulazimisha sana.Unajiuliza maswali kwanini nimechelewa kumpata huyu siku zote hizo.
Mnapanga kuoana.Una kwenda kwao kutoa posa majibu ya barua ya posa unaambiwa utoe mahali ngombe wanne,majembe 5,Pesa taslimu milioni tatu na uandae koti la babu,Blanket la shangazi,malipo ya mama mlezi milioni moja na makolokolo mengine ambayo yanahitaji ushinde biko au tatu mzuka ndio uyashinde.
UNGECHUKUA UAMUZI GANI BAADA YA HAYO KUKUTOKEA