johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 94,182
- 164,685
Nimeambiwa Iringa ni mkoa pekee Tanzania wenye kabila mwenyeji moja tu WAHEHE,je ni kweli?
Nimeambiwa Iringa ni mkoa pekee Tanzania wenye kabila mwenyeji moja tu WAHEHE,je ni kweli?
Wasagara?!!kabila hili ndio leo unanijuza,ahsante.Iringa kubwa, kuna Iringa Mjini hapa hakuna mwenyeji bali ni wenyeji mchanganyiko.
Kuna Iringa Vijijini huko ni makabila mchanganyiko(Wadzungwa Utawakuta Kilolo, Wahehe hawa utakuta sana Kalenga, Wasagara utawakuta sana Ruaha Mbuyuni, Wabena utawakuta wachache Isimani)
Kuna Wilaya ya Mufindi hapa ndio utawakuta Wahehe wengi na Wabena.
Hakuna Mwenyeji bali kuna Wenyeji .
Hata wachaga?makabila yote uliyoyataja ni wenyeji wa Iringa.
Nadhani anamaanisha wang`anzagara na sio wasagaraWasagara?!!kabila hili ndio leo unanijuza,ahsante.
Aisee Tanzania kuna makabila!Nadhani anamaanisha wang`anzagara na sio wasagara
Ni rahisi mtu kusema Iringa inakaliwa na wahehe tu, ila ukiingia ndani zaidi utakuta kuna minor variations... Kuna wahehe ambao ni wengi zaidi katika wilaya zote (Mufindi, Kilolo na Iringa), lakini pia kuna jamii za wakinga, wabena, wapangwa ambao asili zao ni Njombe, Makete na Ludewa,Nimeambiwa Iringa ni mkoa pekee Tanzania wenye kabila mwenyeji moja tu WAHEHE,je ni kweli?
Waburushi bado wapo?kuna kipindi walikuwa wengi sanaNi rahisi mtu kusema Iringa inakaliwa na wahehe tu, ila ukiingia ndani zaidi utakuta kuna minor variations... Kuna wahehe ambao ni wengi zaidi katika wilaya zote (Mufindi, Kilolo na Iringa), lakini pia kuna jamii za wakinga, wabena, wapangwa ambao asili zao ni Njombe, Makete na Ludewa,
Zaidi ya hapo kuna mwingiliano mkubwa wa kijamii wa toka enzi, kiasi kwamba huwezi tofautisha sana Mbena na mhehe, labda kidogo mkinga na ndio maana wengi huita tu wahehe , ila kiuhalisia it is not really. Na pia kuna jamii za watanzania toka mikoa mingine ambazo zimefanya makazi hapa, kwa ujumla huu mwingiliano umefanya hybridization nzuri katika hizi jamii.
kiasili na kiumiliki, iringa ina kabial moja tu ila lina vimatawi vitatu. kuna wahehe halisi (kalenga, isimani, mufindi, ifunda, hadi ilula), wengine ni wadzungwa (hawa wanapatikana wilaya ya kilolo,kihehe chao ni tofauti kidogo na hiki cha mkwawa, wao wanaenda deep zaidi kwasababu ni waporipori na watu wa milimani zaidi, primitive zaidi yaani), na tatu, kuna wasagara ambao ni wahehe wa maeneo ya ruaha mbuyuni, mahenge etc, hao ni wachache sana na ni kama hawatambuliki kabisa. wanaotambulika ni wahehe halisi hawa wala mbwa, na wengien wahehe wa udzungwa. huo ndio ukweli nilioupata kwa bibi yangu na kwa kushi kwangu iringa kwa miaka 14Iringa kubwa, kuna Iringa Mjini hapa hakuna mwenyeji bali ni wenyeji mchanganyiko.
Kuna Iringa Vijijini huko ni makabila mchanganyiko(Wadzungwa Utawakuta Kilolo, Wahehe hawa utakuta sana Kalenga, Wasagara utawakuta sana Ruaha Mbuyuni, Wabena utawakuta wachache Isimani)
Kuna Wilaya ya Mufindi hapa ndio utawakuta Wahehe wengi na Wabena.
Hakuna Mwenyeji bali kuna Wenyeji .
kiasili, Iringa kwa sasa ni mkoa wa Wahehe. ukitaja wadzungwa na wasagara ambayo ni matawi ya wahehe, wote hao wanaongea lugha ile ile ya kihehe tofauti ni lafudhi tu, sawa na wanyakyusa wa kyela na wa tukuyu. ila kuna wahamiaji ambao ni wabena wengi sana, wakinga wachache na makabila mengine. kwa wale tusiosoma iringa tukutane hapa.kiasili na kiumiliki, iringa ina kabial moja tu ila lina vimatawi vitatu. kuna wahehe halisi (kalenga, isimani, mufindi, ifunda, hadi ilula), wengine ni wadzungwa (hawa wanapatikana wilaya ya kilolo,kihehe chao ni tofauti kidogo na hiki cha mkwawa, wao wanaenda deep zaidi kwasababu ni waporipori na watu wa milimani zaidi, primitive zaidi yaani), na tatu, kuna wasagara ambao ni wahehe wa maeneo ya ruaha mbuyuni, mahenge etc, hao ni wachache sana na ni kama hawatambuliki kabisa. wanaotambulika ni wahehe halisi hawa wala mbwa, na wengien wahehe wa udzungwa. huo ndio ukweli nilioupata kwa bibi yangu na kwa kushi kwangu iringa kwa miaka 14
Inasemekana hakuna kabila la wahehe, ila kuna hayo makabila mengine ambao wakati wa vita (na wajerumani kama sijakosea basi ni vita na makabila mengine) walikuwa wakisema he!! he!! he!!! kama njia ya kutishia na kutiana ujasiri wakutanapo na maadui kwenye uwanja wa mapigano, ndipo wote bila kujali walitokea maeneo gani wakaitwa hehe, lakini kiuhalisia walikuwemo wadzungwa, wasagara na hata watu wa kutoka ujombani kwa Mkwawa walikuwemoIringa kubwa, kuna Iringa Mjini hapa hakuna mwenyeji bali ni wenyeji mchanganyiko.
Kuna Iringa Vijijini huko ni makabila mchanganyiko(Wadzungwa Utawakuta Kilolo, Wahehe hawa utakuta sana Kalenga, Wasagara utawakuta sana Ruaha Mbuyuni, Wabena utawakuta wachache Isimani)
Kuna Wilaya ya Mufindi hapa ndio utawakuta Wahehe wengi na Wabena.
Hakuna Mwenyeji bali kuna Wenyeji .
ukisoma historia ya mkwawa (nimetoka kuisoma hapa), hao wahehe wote chini ya mkwawa, walikuwa na koo zao kabisa, hawakuwa watu mbalimbali ila watu wanaojuana kwa koo. mamangu ni mhehe, hadi leo, kwenye koo zao ili wasioleane ndani ya damu, wana miiko fulani, mfano, mamangu ni mwiko kula sungura na ukoo wake wooote hawali sungura, hivyo wakikutana huulizana mwiko wako nini, wanajuana kuwa ni ndugu. ukisoma historia utakuta wale wa kilolo walikuwa na koo kama mihafuwa n.k, iko wazi. uliuwa ni utawala real kabisa na wenye watu distinct.Inasemekana hakuna kabila la wahehe, ila kuna hayo makabila mengine ambao wakati wa vita na wajerumani walikuwa wakisema he!! he!! he!!! kama njia ya kutishia na kutiana ujasiri wakutanapo na maadui kwenye uwanja wa mapigano, ndipo wote bila kujali walitokea maeneo gani wakaitwa hehe, lakini kiuhalisia walikuwemo wadzungwa, wasagara na hata watu wa kutoka ujombani kwa Mkwawa walikuwemo
Nami nilikuwa nafahami hivyo japo siyo in detail kama ulivyoeleza, lakini kuna Mzee mmoja wa ukoo wa akina Muyinga kama sijakosea alisema hao wote ikiwa ni pamoja na wazazi wa akina Mkwawa wenyewe ni kwamba kuna sehemu walitokea katika kuzaliana kwao ndipo zikaanza kupatikana hizo koo katika maeneo yanayoizunguka Iringa na Iringa yenyewe.ukisoma historia ya mkwawa (nimetoka kuisoma hapa), hao wahehe wote chini ya mkwawa, walikuwa na koo zao kabisa, hawakuwa watu mbalimbali ila watu wanaojuana kwa koo. mamangu ni mhehe, hadi leo, kwenye koo zao ili wasioleane ndani ya damu, wana miiko fulani, mfano, mamangu ni mwiko kula sungura na ukoo wake wooote hawali sungura, hivyo wakikutana huulizana mwiko wako nini, wanajuana kuwa ni ndugu. ukisoma historia utakuta wale wa kilolo walikuwa na koo kama mihafuwa n.k, iko wazi. uliuwa ni utawala real kabisa na wenye watu distinct.
ila hao cha muhimu ni kwamba hao jamaa hadi leo wana koo identical za tangu enziNami nilikuwa nafahami hivyo japo siyo in detail kama ulivyoeleza, lakini kuna Mzee mmoja wa ukoo wa akina Muyinga kama sijakosea alisema hao wote ikiwa ni pamoja na wazazi wa akina Mkwawa wenyewe ni kwamba kuna sehemu walitokea katika kuzaliana kwao ndipo zikaanza kupatikana hizo koo katika maeneo yanayoizunguka Iringa na Iringa yenyewe.