Siyo kuwa nimechezea cha mpavu! Nimejaribu kuwa ninasoma POSTS zinazochapishwa humu Jf, hasa Love Connect, na nimegundua kuwa wanaokuwa wanachapisha posts ni watu walewale ila wanabadilisha ID zao. Hivyo, naamini kuwa wanawapata wanaume au wanawake halafu pengine unakuta mtu alivyotarajiwa sivyo inavyokuwa. Mimi ni msomaji tu wa POSTS za humu ndani na wala siwezi kutafuta mwanamke kwa njia ya mtandao. Mimi mwanamke wangu tayari ninaye na nimedumu naye kwa muda wa miaka minne na nusu hadi leo. Hivyo, mimi ninawapa ushauri tu maana naona kwa muda mrefu wanaoleta machapisho ni walewale ila kinachobadilika ni IDs zao tu.