Wengi hatusali kwa Imani, Tunasali tuonekane

Sinywalulenga Muvina

Senior Member
Jun 14, 2013
124
62
Kichwa habari kinahusika!

Tumezoea kuna katika mitaa yetu, kuna baadhi ya watu wanafahamika sana kwa kuhudhuria nyumba za ibada. Na huheshimika sana hata akisema jambo flani kwa sababu anaonekana ni mtu msafi na mcha Mungu.

Lakini kuna wengine ni wezi, wazinzi, matapeli, waongo, wakatili, roho mbaya n.k. na wanatumia kufanya ibada kama kichaka cha kujificha ili ikitokea wakajulikana mabaya yao, jamii husika imtetee na kumuonea tu huruma. Hawa hawakosi nyumba za ibada, na wanahakikisha wanaonekana na kila mtu aliyepo eneo la ibada. Na wanatoa sana misaada kwenye nyumba za ibada.

Hilo si jambo zuri sana na ni chukizo mbele za Mungu kutumia nyumba zake kama kichaka. Mbele ya binadamu utaaminika ila hujui ni adhabu gani utaipata baada ya maisha ya hapa duniani. Ni vema kuishi sasa tukitengeneza maisha ya furaha ya milele baada ya kuondoka katika safari ya hapa duniani.


NB: Katika kipindi hiki ambacho kuna madhehebu ya kikiristu wanafunga kwa ajili ya msamaha wa dhambi, niwasihi kuwa kufunga ni jambo jema, lakini kufunga kunakoambatana na kusaidia wasiojiweza, kusaidia yatima, kutembelea wagonjwa na kuwasaidia pamoja na kuwatembelea wafungwa magarazani ni mambo mazuri zaidi.
Vitabu vya Mungu vinahimiza kuwatembelea na kuwasaidia wenye uhitaji kila mara, hasa Yatima, wagonjwa na kuwatia moyo walioko kwenye magereza.

Tuache kusali kwa kuonekana na watu. Kusali kwetu kuwe ni siri kati yako na muumba wako, maana yeye anakujua vizuri kabla hujazaliwa.

Tuache kupenda kusali mahala flani kwa sababu tutaonekana kwenye Tv, na watu watajua tunasali huku tukiendelea kutenda mabaya, hatusamehi, tuna vinyongo, tuna roho mbaya mbele ya binadamu wezetu. Hakika hasira za Mungu zitakuwa juu yetu.

Tufanye kila kitu kwa roho nzuri, na tupende kuwa wasafi wa mioyo kila wakati maana hatujui siku wala saa ya kifo chetu.

Niwatakie wakati mzuri!
 
Kuna hawa wanaojiita Walokole; Sijapata kuona watu wenye Roho Mbaya, chuki, utengano na Uadui kama wao. Ole wako uwe na Boss Mlokole hutakaa ujiunge nao! Kwa matendo yao ya Roho mbaya.
 
Mkuu Inanambo, ndiyo maana nimesema kuwa wengi tunatumia imani kama vichaka, ila mioyo yetu haiko safi. Ni wabaguzi, wabinafsi n.k. wengi ni wabaguzi sana kwa watu wasio wa imani yao. Sasa sijui ni wapi walifundishwa hivyo. Maana vitabu vyetu vya dini vinatuambia tuwe na upendo kwa watu wote
 
Back
Top Bottom