Wema Sepetu anafaa sana kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa.

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
Kutoka FB:

WEMA SEPETU ALIFAA SANA KUWA Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

Tatizo la CCM wao wanafikiri kuongea kwenye TV ndio sifa, wao wanafikiri Critical Thinker ni mpaka uwe mbunge au mjumbe wa bunge la Katiba au......au mtoto wa Fulani.

Misingi ya Mwalimu haikuangalia wewe ni nani, Bali iliangalia watu wanaoweza kukivusha chama.

Wema ana sifa zote na ndio maana kaanza kuchafuliwa, Wema ni mdada mbunifu anawafaa sana wana CCM.

Chama tarajiwa cha ACA kinawatakia Heri ya miaka 40 ya kuanzishwa kwa CCM.

Deogratius Nalimi Kisandu
Mtemi Kiongozi wa ACA tarajiwa.
 
Kutoka FB:

WEMA SEPETU ALIFAA SANA KUWA Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

Tatizo la CCM wao wanafikiri kuongea kwenye TV ndio sifa, wao wanafikiri Critical Thinker ni mpaka uwe mbunge au mjumbe wa bunge la Katiba au......au mtoto wa Fulani.

Misingi ya Mwalimu haikuangalia wewe ni nani, Bali iliangalia watu wanaoweza kukivusha chama.

Wema ana sifa zote na ndio maana kaanza kuchafuliwa, Wema ni mdada mbunifu anawafaa sana wana CCM.

Chama tarajiwa cha ACA kinawatakia Heri ya miaka 40 ya kuanzishwa kwa CCM.

Deogratius Nalimi Kisandu
Mtemi Kiongozi wa ACA tarajiwa.
Atakuwa anaeneza itikadi gani? Labda ngada kama ipo kwenye ilani ya chama chake!
 
Mkuu hicho chama mapato yake mengi yanatokana na ngada, ndio maana hawajali lolote kuhusu waasirika wa madawa ya kulevya.
And good enough wapiga kura wengi wa chama chao ni hawa hawa mateja...mi nasema ni mbwa kala mbwa baaaas!
 
wana hasira nae sana alipiga hela nyingi sana wakati wa kampeni wakati mzee kinana alikuwa analima huko vijijini wema anapiga selfie tu ndani ya magar akiwa katupia gwanda la kijani mjini mipango
 
Wauza unga wengi wako ndani ya ccm


=======================================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Sina muda kujadili upuuzi huu kuhusu Ridhiwani &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Rais Jakaya Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni mkusanyiko wa upuuzi mtupu madai kuwa yeye Rais alishiriki kumwokoa mtoto wake, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete ambaye alikuwa amekamatwa na madawa ya kulevya nje ya nchi.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Urais ni taasisi kubwa sana nchini na hivyo yeye akiwa Rais hawezi kujiingiza katika ubishani na watu wa mtaani, kama ambavyo wanataka baadhi ya watu wanamsukuma ili ashiriki katika maneno hayo ya mitaani.

"This is nonsense &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; ni mkusanyiko wa upuuzi. Sina muda wala siwezi kupoteza nguvu yangu kujadili upuuzi na ujinga wa namna hiyo," amesema Rais Kikwete usiku wa Jumamosi, Agosti 2, 2014, wakati alipozungumza na Watanzania wanaoishi katika Marekani kwenye Hoteli ya Marriot Washington, mjini Washington D.C.

Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku tisa katika Marekani alitoa majibu hayo baada ya kuwa ameulizwa kuhusu madai yaliyotolewa Julai Mosi, mwaka juzi, 2012 na Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA, Wilbroad Slaa, madai hayo yamempeleka mahakamani.

Amesema Rais Kikwete: "Hatuwezi sisi kujiingiza katika shughuli ya kupoteza muda kwa kushiriki upuuzi na ujinga. Haya ni maneno ya kipuuzi yanayosemwa na watu ambao kazi yao usiku na mchana ni kuota jinsi ya kuyumbisha ajenda yetu ambayo imefanikiwa sana katika kubadilisha hali ya maisha ya Watanzania.'

Amesisitiza Rais Kikwete: "Urais ni taasisi kubwa sana. Rais wa nchi yetu hawezi kujiingiza katika ubishani na watu wa mitaani. Kwanza huyo Ridhiwani amemfikisha Slaa kortini na mpaka leo hata kesi yenyewe haijatajwa."

Kuhusu swali jingine aliloulizwa kuhusu suala hilo, kuwa Rais Kikwete alitia saini mikataba 12 na uongozi wa Jamhuri ya Watu wa China kama sehemu ya masharti ya kuachiwa kwa Ridhiwani, Rais Kikwete amesema:

"Naipenda nchi yangu kiasi cha kwamba siwezi kufikiria hata kuiweka rehani. Haya ni maneno ya kipuuzi tu, yenye kutafuta kututoa kwenye ajenda zetu nzuri. Hatuna muda nayo, sisi tunaelekeza nguvu zetu kwenye mambo ya maana ya kuleta mabadikio katika ustawi wa Watanzania."

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Dar es Salaam.
04 Agosti, 2014


Swissme
 
Hivi vyama vya upinzani ni shiida
Mara mfalme kiongozi Mbowe
Hatujakaa sawa anakuja Mtemi kiongozi Kisandu!!!!
Lini Mbowe Kawa mfalme kiongozi je lini chadema ikaweka hicho kipengele cha uongozi kwenye katiba yao? Na Mbowe kaingiaje kwenye hii mada? Mbona hujagusia mtukufu kiongozi magufuli? Wewe ni kimada wa Mbowe labda kakutelekeza ndo maana unamuingiza kwenye mada zisizomhusu.




By Kamanda wa KIRIBA kwa sasa ARUSHA
 
Back
Top Bottom