ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,592
Habari wanajamvi wenzangu
Natumaini mko fiti ktk weekend hii, wengine mmepumzika kutokana na wingi wa shughuli za wiki iliyopita, na wengine mko pande tofauti mkisalimia ndugu na jamaa na marafiki zenu pia, ila wengine sasa mko sehemu ambazo hazimpendezi Mungu hizo siwezi kuzitaja kwani wenyewe mnazijua,
Awali ya yote ningependa kuwashirikisha jambo hili hasa kwani lilikuwa limenigusa sana muda mrefu na nika sema ipo siku nitawashirikisha marafiki zangu wa jf hasa hapa katika jukwaa la CC kama tunavyolifupisha.
Jambo ambalo ningependa kuwashirikisha hili Je rafiki yangu umevipa kipaumbele vitu gani hasa katika maisha yako ya kila siku, Je umetoa muda gani kwa mambo ya muhimu ya kuyafanya ukiwa ungali unaishi mpaka sasa? Je ni kitu gani umekipa umuhimu wa kwanza kukifanya kuliko vyote ambavyo umevipanga kwa mwaka huu kufanya? Na je kama bado unasubiri nini ufanye na wakati tumeshaifikia robo mwaka ya 2013 utafanya lini? Je unajua wakati haukungoji unasubiria nini hasa?
Maswali yote haya nadhani utakuwa na majibu yake au umeshajua ni kitu gani nataka kueleza hapa, kitu kilichonigusa moyoni mwangu mpaka kutoa thread hii ni changamoto za maisha ya sasa jinsi yalivyo, yamepelekea hata watu kujiuliza ni lini wanaweza kutoka kama Mtambuzi alivyotoka na kufungua kitu chake, Wengi wanajiuliza ni lini nitatoka hapa nilipo sasa, na kuweza kujikwatua kila mahali, wengi wameshatoka ila bado wajaweza kutoa kipaumbele kwa yale mambo ya muhimu kwao kufanya wakati huu.
Kwanini nimesema haya hapa ni kitu gani haasa umekipa kipaumbele kwa maisha yako ya sasa? Je kimwili ni kitu gani hasa ni masomo, kazi, biashara, ujasiliamali, au nini hasa? na upande wa kiroho ni kitu gani umekipa kipaumbele zaidi ambacho chaweza kutokea hata katika kizazi chako hapo baadaye nao wakarithi hicho, Je ni huduma, utumishi, kuwa paroko, kuishi maisha yampendezayo Mungu, kumtumikia kwa kila hali na mali zako? Nini hasa Rafiki yangu umefanya kiwe cha muhimu zaidi. Ona mfano huu ambao tunaona watu ambao waliishi pasipokuweka vitu vya muhimu kwao yaani waligongana na huduma Yesu kipindi kile alipokuweko duniani
Mfano halisi ni huu ukisoma katika Matendo 1:6-8wayahudi walikinzana na Yesu wao walijua kuwa wamerudishiwa utawala wao toka kwa Warumi waliowatawala na kumbe ilikuwa ni vise versa kwa Yesu kwani Yesu Kristo aliwaambia kuwa yeye anapaa na atawaachia Roho Mt. kuja kuwa msaidizi kwako huo ni ukinzani yakinifu kwa watu wengi sana hasa hata kipindi hichi cha kwaresma
Mfano mwingine tunaona katika huduma ya utumishi wa Yesu alipokwenda kwa mfarisayo kumtembelea akatokea mwanamke kahaba aliyekuwa akiishi maisha ya dhambi, na anasa za dunia hii alipomwona Yesu pale akaenda miguuni pake akalia sana akiomba msamaha kwani alitambua na kujua yu mkosaji kalia miguuni pa Yesu na kufuta miguu kwa nywele zake na kisha kuchukua kibweta cha mafuta mazuri na kumpaka Mfalme Yesu alijua kwanini alifanya vile ni kutoikana na kutambua yu mkosaji na lifanyaa vile cause mambo aliyoyafanya huko nyuma. Yuda alipomwona alisema huyu mwanamke anaharibu hayo mafuta yenye thamani kubwa sana si angeuza na tukawapa maskini? Yuda akutambua kuwa yule mwanamke aliweka kipaumbele cha moyo wake kwa Yesu hakuona umuhimu wa mafuta mazuri ya marhamu aliona uthamani wake ni kuyatoka maisha yake na kutubu dhambi zake kwa Yesu kristo, ndipo Yesu alitambua kuwa yule mwanamke aliweka kipaumbele kipi akamwambia mwanamke imani yake imeponya. Je wewe rafiki uyangu umeweka kipaumbele kipi katika maisha yako ya kiroho hapa duniani, Je unaona unaishi tu kwa kwenda mbele. Hebu jichunguze na anza sasa kuweka kipaumbele kwa mambo yako ya kiroho. na kimwili pia.
Hebu rafiki yangu achana na dhani ya kusema bora liende kutokuwa mtu wa kuvipa umuhimu vitu vya muhimu kwako yaani vya kwanza,. Usiishi maadamu unaishi tu uwe na malengo ya nini cha kufanya hasa kijana mwenzangu, usitoe nafasi kwa vitu visivyofaa wekeza katika kuufikia malengo yako ya mwaka huu na mstakabali wa maisha yako utabadilika ikiwa wewe utabadilika katika ufahamu wako. HEBU WEKA NIA YA KUUFIKIA MALENGO YAKO NA WEKA KIPAUMBELE KWA MAMBO MUHIMU
Copy: Bakulutu, Mentor, watu8, Erickb52, Bujibuji. snowhite, Mamndenyi, stevoh, Nicas Mtei, Donn, Dio, charminglady, gfsonwin. Arushaone, Excellent, nitonye, Madame B, Chimbuvu, Mr Rocky, Invisible, FirstLady, Pascal Mayalla, MAMMAMIA, Bundewe, Filipo, Zion Daughter, Baba V and all jf cc,all jf friends :frusty::ranger::fish2::drum::behindsofa:😛opcorn::bathbaby::ban: chagua kimojawapo
Nakutakia jioni njema

Last edited by a moderator: