Weekend story! BEN 10

Nani mwingine ameyaelewa maombi ya Ghost kwa Mungu, Yaani nimecheka mno eti Mungu nakujengea makanisa na kusomesha yatima wako na kuuza unga kidogo tu LOL.

Story za Lara1 ukidhani hii ndo the best of all akileta nyingine ana outdo unajikuta kila story ni best ukilinganisha na nyingine. Personally nishachoka kumsifia fanani apambane na hali yake tu sa hivi.
 
Najua mshapata upande mmoja wa story yangu ya kufumaniwa! Nasisitiza msomaji huo ni upande mmoja tu! Na umeletwa kwa lengo la kunichafua na kuninyongonyeza! Na kunifanya nionekane sina thamani, wala sina maana yoyote!

Mwanzo kabisaa niliolewa out of fear na stigma huenda bikaishia peke yangu! Maana kasumba kasumba hizi! We kataa wanaume wa maana, wanapoteaga hawa! Utakosa hata wa kukupa mambo! We jitie mchagua sanaa! Mwisho utachagua koroma!

Hizi tantalila zikaniingia nikajikuta tu nipokwenye kona nalazika kufanya mamuzi magumu! Moyo haujaridhia ila jamii ndo imenoshika kidete! Maana ilifika stage mashosti wote wameolewa! Kila mtu anaenda kwake kupika! Yuko busy na mume wake! Nikasema hapa sina namna! Sina ujanja! Kuendana na kasi hiisina budi kuolewa! Liwalona liwe!

Kipindi hiko huyu mume wangu kubwa la maadui alikuwa malaya mbwa! Alikuwa na pesa kama yote! Na mimi i was doing more than okay! Nilikuwa nishakuwa head wa idara! Na napokea pesa nzuri! Nishajenga, nishanunua Prado! Kibongo bongo naweza sema nishamaliza kila kitu! Bado tu kuolewa na kuzaa!

Nilikuwa na challange moja! Kila mwanaume anaekuja anakuja kimaslahi! Siku mbili nyingi ashaanza umatonya! Na mimi jamani niwe muwazi kufuga mabwana sio zangu kabisaa kabisaa! Hata paka simfugi mie itakuwa bwana? Thubutuuuuuuu! Bwana akianza tu vizinga kanikosaaa!

Sasa huyu mwakitombile ndo ikawa na nafuu! Japo sasa file lake ndo chafu chafu halifai! Ila financially he was doing more than well! Ana kampuni zake mwenyewe! Na pesa anazo! Na familia yake pesa ipo! Hata akikupa ofa ya outing ni Dubenga, siku ingine Tokyo! Sio mambo ya kitoto!

Watu wananikumbusha mama chamba sanaaa! Chamba mpaka utoke na mavi! We mkaka mzuri, pesa anayo,unachotaka kitugani? Umalaya umalaya kitu gani baba ako mzazi mwenye malaya vile vile ukichunguzakama unabisha muulize mama yako mzazi! We pishana na fuko la pesa kwenye maandamano uone kama atakosa mke!

He was nice to me, and treating me nice! Nikakubali niolewe! Alivokuwa maloveee kipindi chote cha harusi ungemjua sasa? Mpaka kuchagua nguo huyu hapa! Sijui nini huyu hapa! Zikafanyika sherehekama zote! Nikajipa moyo sijafanya makosa!

Maisha yakawa ya kawaida mwanzo! Upendo upo upo kishkaji! Nikazaa watoto wa 3 still we were going strong! Baada ya hapo kurudi ndo saa 5! Ukimuuliza anakwambia nisinywe na washkaji! Kwanza nakuoa nakunywa! Itakuwa sasa! Usinipangie!

Inapita miezi mwanaume hakushikiiii! Hachokozi mechi! Mimi sinyoi na yeye hanyoi! Misitu ya Amazon na Congo! Ukiuliza sababu hamnaaa! Hamna ugomvi useme umuombe mtu msamaha hamnaaa! Imetokea tu!

Ukiulizakwawengine wanakwambia wembe ni ule ule! We mwezi tu hajakugusa mie nina miaka mi 3! Haki nakuapiaaa! Kaka angu yuleee! We mbona una nafuuu kubwa sanaaa! Ndo ndoa hio! Nawaulizasasa wenzangu mnajiburudishaje? Mzee ndo hanihitaji sasa genye zangu nafanya vipi! Naambiwa mtu mzima HAPANGWI! Jiongeze!

Watu hawakupi majibu ya moja kwa moja! Nikawaulizaau niombe talaka yangu? Wakasema alafu? Mitoto mi 3 utampelekea nani? Hio ramani ya kuzimu tumboni nani ataihitaji, na hizo nyama zilizolegea je? Papa hio imepitisha watoto wa 3, kama valuation of assets tunasema SCARP VALUE! We ndo basi ushafeliii! Na huo ndo ukweli! We bana hapo hapo! Acha kuwa postive! Think of your mother! She stayed with pops not because she loved him, she had no where to go na nyie! Overtime nafsi itakomaaa! Utazoea!

Nawaa!bia hapana aisee! Why do we have to end up like this? Mmmmmmh! Wanaguna! Wanakwambia huko nje kumebadilika! Sio kama ulivokuacha! Sahivi hata wewe ukimtaka kijana umlipe wewe! Umgharamie ndo aingize kojoleo lake akojoe! Ama sivo uibe mabwana za watu, na wakikumata wenywe topaz za uso tu kukuhusu! Bora uendelee kumbembeleza mumeo akufanye hivo hivo hata kwa kungangania!

Think on the bright side! Unajitamba mbele za watu una mume! Umepata wa kukustiri! Una familia! Watu wakiongea familia fyoko fyoko unayo pia! You basically have it all on the outside! Japo u ajua on the inside you have nothing! Who cares? Either way life facks us all!

Nawaambia huyu bwana hawezi kuwa ankaa miezi yote hii hana mwanamke uko nje! Lazima ana mwanamke nawaambia! Naambiwa unauliza majibu! Pigia jibu mstari funga kitabu! Ukisema ukichokonoe utayapata mazito kuliko unayotafuta! Unaweza kukuta mumeo hana wanawake hukonje ila ndo yeye mwenyewe anageuzwa mwanamke! Mwana kulitafuta mwana kulipata! Tuliza mishono mitatu hio lea watoto hao!

Nikaanza kuongea na mume wangu kidiplomasia? Nini tatizo? Nini kimebadilika? Mbona hakuwa hivo! Kama nimekukosea nisamehe! Anasema unapenda sanaa drama! Na mapenzi ya tamthilia! Sisiwazazi sahivi! Tushapita huko! Mara unapenda mapenzi ya kugeza sanaaa!

Nawauliza wenzangu nini kimebadilika! Wananiambia kilichobadilika ulikuwa kijana sasa ni mzee! Afu ubataka upewe wzifa wa vijana! Heheheeee! Kama mazuri vile! Nikambembeleza Mr! twende counseling! Marriage councelling! Akagoma kabisaa! Anasimamia ndoa haina tatizo tatiP ni mimi napenda drama!

Nimevumilia ndugu msomaji miaka kama mi 3! Wa 4 nikaja kufuma sms! Ana mwanamke afu kamjengea nyumba huko Kitunda kubwaa, nzuri hatariii! Nikamsaka huyo mwanamke mpaka nikamjua! Afu mtu mzima sasa! Ana watoto wa 4! Baba tofauti! Hana uzuri wowote ndugu msomaji! Anauza cafe ya chakula! Mama lishe apande juu kidogo!

Niliumiaaa sanaa moyo! Niliumia sanaaaa! Nikaanza kumchatisha kama mkaka nipo bank! Namba si ninayo! Akajaa haraka haraka! Akanielekeza mpaka hapo caffe! Nikaenda! Nikamuangaliaaa! Nikamtumi sms acha kutembea na waume za watu! Nitakitia ki cafe hiko kiberiti! Akajibu mumeo atanifungulia ingine kama alivonifungulia hii! Jeuriii ndugu msomaji! Navowaambia jeuri hamjamjua kabisaa!

Nikapata ujasiri wa kumuuliza kwani mume wangu unampa nini lakini? Akajibu hata nikikwambia jeuriya kumpa hiko nachompa unayo? Nikamuuliza nini unampa acha kuzunguka! Akajibu Matakoz! Mpe na wewe kama unaona rahisi atatulia kwenye ndoa kama maji ya mtungi heheheeeyaaaa!

Nikaona napoteza tu mda! Bwana nilimshika mashati si kidogo! Nikamwambia naondoka na wanangu! Akasema ukiondoka namuha!ishia humu ndani kama unataka kutukomoa bora tu ubakie! Nishakwambia nilipitiwa nitajirekebisha! Nikajipa matumaini anajitutumua tu ila atajirekebisha!

Kweli lileshangingi aliachana nalo! Manake likawalina ni text naona unaloga sanaa siku hizi kuniharibia! Sijui unalala na mganga! Heheheee! Nikajua ashaachika! Nikamjibu cha kuazima hakistiri wowoo! Asharudi nyumbani. Na matusi tukawa tunafanya kama kawaida! Upendo ukarejea!

Miezi mi 3 mingi! Ratiba zikarudia pale pale! Nikajaribu kujua anatembea na nani? Sikuwezakujua kabisaa! Nikakata tamaa! Nikawa nimejikalia nasononeka tu! Nikaja kupenyezewa anatembea na ndugu yake! Wa mbali ila udugi wa kuvuta manati upo! Nikamuuliza akaniambia wewe ni pumbavu kabisaa! Nikatembeee na ndugu yangu ili? Hata kama umaluuni ndo nimekosa kabisaaa kiasi hiko? Hataaaaa! Haiwezekani! Nikamuamini asilimia 100. Ikaja baadae kujulikana tena na mume wa huyu ndugu! Ilikuwa aibu ya kufungia mwaka ndugu msomaji! Alirudi nyumbani mikono nyuma!

Akaanza kutembea na binti wa 18 yrs! Msomaliiiii! Kadogo kakorofiiii Alshababu wa kike! Huyu ndo hajifichi kabisaa! Anawambia wanangu yeye anti! Mwambieni mama yenu anti anawasalimia! Kwanza sikutaka kufanya nae ligi sababu ni mdogo sanaa! Ningeweza kumzaa kama ningeamuaga kuzaa na miaka 16! Afu design nishachokaaa! Najua akitoka huyo ataokota mwingine! Nikakubali tu matokeo!

Akamtia mimba yule msomali akampangishia! Akawa ndo mke mdogo tena! Miminavumilia tu ndugu msoaji! Moyo ukawa u ejaa sumu! Sumu kaliii! Mpaka nikaanza kuumwa pressure! Watu waka ipeleka kwe ye maombi! Maombi yalinisaidia kusamehena kurejesha amani na pressure ikaisha kabisaa!

Nimezunguka makanisa mengi sanaa! Mpaka kufika kwa pastor! Pastor mara ya kwanza nawaona na mkewe kiukweli walinivutia! Anajua thamani ya mke! Anampa mkewe nafasi! Wanavosema apatae mke kapata kitu chema basi anavokienzi sasa! Mwanaume ndo yule!

Akaanza kunipa huduma! Wanangu wako boarding wote, Mr ndo vasco da gama! Nikamjaza mimi single mother! Huku na huku tukaanguka dhambini! Mkewe aliistukia! Na mimi sikuachia sababu na mimi nporwa mume natulia! Nabebewa mume natulia! Na safari hii mwenye mume atulize kitenesi!

Kama biliwaza danger ya fumanizi labda upande wa Mozah! Sio mume wangu! Maana ashanichoka na kunisusa kabisaakabisaa! Sikuwaza kwamba mimi kuchepuka kutamtoa roho kiasi kile! Sikuwahi kuwaza! After all the cheatings nilizomkamata sikutegemea angenivua nguo kiasi kile! Tuna watoto wakubwa! Uzuri wako nje! Na aliwahonga gazeti wamsanue pastor sanaa mimi wafunike funike! Hata sura yangu haikutoka! Wala kazini hawakijua! Still it was inhuman!

Yeye akanipa talaka akajua kanimaliza! Mimi nikaenda mahakamani kufungua kesi rasmi ya talaka na tugawane mali! Hapo kwenye kugawana mali palimvuruga sanaaa! Akakimbilia kwa paroko tusuluhishwe ndoa za kikristo hazina talaka! Paroko akaniandikia wito mara 3 wa kuitwa parokiani! Sikwenda! Akamtuma mwenyekiti wa jumuiya! Nikamwambia nimeokoka sahivi so automatically sio kondoo wake!

Mimi nimeweka wana sheria law firm! Na pendekezo langu nipewe 80% ya mali na custody ya watoto! Nika sight kuzaa nje kwamba kaoa mtu mwingine kiserikali ana ishi nae! Akaona kesi imemkalia vibaya! Akaja kidiplomasia! Anasisitiza watoto watoto! Akaomba msamaha hasira tu! Akaomba anipe mali kiduchu tuyamalize kishkaji! Nikamwambia tukutane mahakamani! Mchaga alidataaaa!

Mlokole kiukweli baada ya tukio alisikitisha sanaa! Mozah alimfukuza nyumbani! Kumbe nyumba wanayoishi ni ya Mozah! Nikampa pesa akapange hoteli ya gharama! Ananiambia siwezi kurudi madhabahuni naomba nitafutie
mtaji wa biashara yoyote!

Msomaji kama mjuavyo sifugi mabwanaa mimi!Kila sms akituma anaomba pesa! Kama mimi ndo nimemzaa vile! Alinichosha sio kidogo! Nifanyie hiki nifanyie kile! Like seriously! Utetezi wake siwezi kupanda madhabahuni! Nikamwambia inaweza kupanda vizuri sanaa! Akasema siwezi gazeti limesambaa nchi nzima!

Nikamwambia kwani mbona wenzio wanasimuliaga nilikuwa jambazi! Nilikuwa kibaka, nilikuwa jela ndo wokovu ukanijiaaa! Na waumini tunatoa Amen za kutoshaa tu! Sasa wewe utasema Nilikuwa Mzinzi, muasherati kasingiziwa! Nikafumaniwa na mke wa mtu, na kuandikwa gazetini! Tafuta gazeti la tarehe flani na mwaka flani utaniona front page! Lakini bwana kaniletea wokovuuuu! Haleluyaaaah! Sasa nahubiri neno! Mbona Amen zitakuwa za kutosha tu?

Anajitetea pale, shida yake asifanye kazi aishi kwa mgongo wangu! Aaaah subutuuuuuuu! Nikaona hatuelewani! Nika mblock! Akawa hana pa kunipataaa kabisaaa! Atanipatia wapi mie mtoto wa mjini? Kama Mozah ndo alikuwa anmfuga ni Mozah huko huko sio mie! Kabisaaa!

Woga tu ndugu msomaji ndo ulikuwa unanirejesha nyuma! Kesi yangu inanguruma! Nikaanza kutongoza vikaka vya bank! Hawa njaa kali! Nikampata mmoja! Kimuonekano ana njaaa na nilitegemea ana njaa! Lakini nimeanza kutoka nae hakuwahi kuniomba kitu! Labda mimi kwa nafsi yangu ndo nimpe!

Mwenyewe kwa kujisikia tu rohoni mwangu nikampatia MarkX, nikampangia na appartment niwe najiachia huko! Mtu wa bata sanaaa! Na mimi watoto wakubwa sina majukumu basi tunajiachia wote sanaa sanaaa! Burudaniii! Watu ofisni wanaongea, lazima waongeee si unajua jelousy, ila sisi hatuna habari!

Siku tunatoka kwenye bata akawa ana search station nikasikia kama sautinaijuaaa! Nikamwambia acha hapo hapo! Ilikuwa Wapo Radio! Nikasia " Mimi nilikuwa mzinzi tena muasherati kweli kweli, nishafumaniwa na mke wa mtu na picha kusambaa magazetini ila leo Nawtangazia wokovuuuu! Ameeeen! Ameeeen! Yesu huyuhuyu alieniokoa mimi mkaribishe kwenye maisha yako! Haleluyaaah! Ameeen! Za kutosha kabisaa!

ITAENDELEA!
 
ahahahahahahahhahahahahahhahahhaahah hakyanani mi nilikuwa mzinzi sanaa! muasherati sanaa! lakini nimeokoka now!
AHHAHAHA hii confession mbn huwa siioangi kwenye TESTAMONIES!
 
Jkk
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimelitafuta hili goma nikajua nitakuta limependeza!
Fanani mbona unatufanyia hivi lakini!?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…