We dada wa ndoa nisikilize

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
Wakati huu ambao unajiona wewe umekua na huwezi kumfanyia mumeo yale mambo yaliyokuwa yakimvutia kipindi alichokuwa anakunyapia, ujue ndivyo unavyozidi kutoa nafasi kwa wasichana wengine kumfanyia mumeo mambo hayo hayo ambayo wewe unayohisi ni ya kitoto kwako.

Kama ilivyo kwa wanawake kupenda kudekezwa, kupetiwa petiwa, kubembelezwa nk, ndivyo ilivyo kwa wanaume kupenda kuheshimiwa, kunyenyekewa na kubwa zaidi mume anahitaji ushawishi mkubwa wa kihisia na uhamasishaji mkubwa wa tendo la ndoa kutoka kwako, kitu ambacho ulikuwa unamfanyia kipindi hamjaingia kwenye ndoa.

Usijione umekuwa na kuizoea ndoa kiasi hicho hadi kufikia mume au wote mkaingiwa na ubaridi katika miili yenu. Usiruhusu hali hiyo ikashika nafasi katika ndoa yako. Mtu wa kwanza anayeweza kufanya mapenzi yakawa moto moto siku zote ni mke hata kama mna miaka 15 katika ndoa yenu.

Mpigie simu au mtumie ujumbe mfupi akiwa huko huko kazi na mueleze kuwa "usiku wa leo unamuhitaji" au mpe ushawishi akiwa huko huko kazi na umwambie kwamba "jana alikufurahisha hivyo ungetamani usiku huu mrudie tena". Vitu kama hivyo vinaweza vikamfanya mume amakinike na wewe kiakili na kimwili, hata kama alikuwa na mpango wa kwenda nyumba ndogo, basi mpango wake utaishia hapo na kukufikiria wewe.

Ila kama unataka kusaidiwa, ishi na mumeo kama kaka yako, mnalala pamoja kila mtu anampa mgongo mwenzie, siku 5 mpaka sita hakuna alie mbusu wala kumkombatia mwenzie. Saa ngapi mume atapata nishati chanya kutoka kwako? Saa ngapi mume tapata joto la mwili wako? Saa ngapi mume atakuwa na hisia za kushiriki tendo na wewe?

Na hali hiyo ya kutokuwa na hisia na kutamaniana ikiendelea katika maisha yenu ya ndoa inaweza ikaleta tatizo kubwa zaidi, ndio pale linapokuja suala la "mume wangu hajiwezi kabisa kitandani yani akishapiga bao moja anageukia upande wa pili".. Atajiweza vipi wakati wewe umeshindwa kumuwezesha.

Kuweni makini katika hilo dada zangu, mume anahitaji sana joto lako, mume anahitaji sana hamasa na ushawishi wako katika tendo la ndoa. Wewe kalia kulalamika hivyo hivyo mumeo hajiwezi, kuna wasichana watawasaidia huko nje na wala wasione huo udhaifu wa waumeo mnaousema.
Nimemaliza kazi kwako
 
Dada wa ndoa

Sent from my ONE TOUCH 4033D using Tapatalk
 

Mbona hii post inatakiwa iwe posted na wanawake. Maana haya mambo ya ndani shekh sisi ni watu wa kusikiliza tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…