WCB wamepataje frequency Dar?

IKIRIRI

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
2,734
Reaction score
3,033
Nakumbuka TCRA waliwahi kusema DSM frequency zimejaa...
Wajuzi naomba ufafanuzi
 
Redio ikianza kuruka hewani hupewa Masafa kwa eneo husika masafa yapo wewe kama una redio njoo nayo utapewa hata 206.8
Jibu nilicho ulizi Tcra walisema dar imejaa
 
Mbona majibu yapo humu JF ndugu mtanzagiza, watu wanazo hizi frequency kitambo sana ukitaka hata wewe ya 90.0 unaipata.
 
Kwenye uzia penyeza rupia watu wengi walinyimwa frequncy mpaka leo ila EFM na WASAFI wamepata kiurahisi..

Hii kitaalamu tunaita kila michezo ina wenyewe
 
Nakumbuka TCRA waliwahi kusema DSM frequency zimejaa...
Wajuzi naomba ufafanuzi
Kwa kawaida TCRA hutangaza pale wanapotoa masafa kwa kampuni fulani. Kwa WCB kuna uwezekano mkubwa wamenunua masafa kutoka kwa mtu mwingine sidhani kama ni moja kwa moja kutoka TCRA
 
kama ilivyo taifa stars na wcb ni national music label so kabla hujauliza upupu uwe unajiongeza sawa we mzee!
 
Hizi frequency za 87.0 fm hadi 99.0fm ni adimu sana kupatikana, na kuna hatari ya muingiliano channel zikiwekwa karibu.Ila wasafi FM wanapiga vyombo mwanzo mwisho
 
Hata Mimi nakumbuka kusikia jambo hilo, kuwa masafa kwa Dar yamejaa, tena wakaanza na utoaji kwa zabuni.
Labda hawa walinunua miaka mitano iliyopita wakahifadhi!
Kuna mtu alinunua pengine akawa ameishikilia, akisubiri aje kuuza kwa bei ya ulanguaji, tena ni watu wa mule mule tcra wanafanya hio michezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…