sonaderm
JF-Expert Member
- Nov 9, 2015
- 618
- 1,816
Miaka kibao imepita lakini sijawahi kusikia madawa yamepungua zaidi ya kuongezeka..Labda ni uwepo wa utandawazi siku hizi ndio umefanya tatizo kuonekana kubwa lakini bado ukweli uko pale pale, juhudi zinazofanywa na ndugu zetu polisi na kitengo cha madawa (Drug enforcement) wako katika wakati mgumu wa kushindwa kupambana na vita hii inayooonekana kuwazidi pumzi!
Nguvu ya pesa imefanikiwa kuwanunua baadhi ya polisi kama Mh. Makonda alivyoelezea jana na inanipa mashaka kama polisi nchini wanayo tena sifa ya kuendelea kupambana na hawa jamaa..
Tukichukulia mifano kama Colombia enzi za Pablo Escobar, serikali ya nchi hiyo ilifanikiwa kumwondoa gwiji huyo kwa operation za kijeshi na za muda mrefu..Nchi kama mexico pia hali kadhalika, jeshi linapewa nafasi katika mapambano hayo kwa kushirikiana na vitengo mbalimbali vya kimataifa vya kudhibit mihadarati..Kwa nini Tanzania kama tumechoka na habari za madawa tusiwakabidhi JWTZ kuwatokomeza hawa jamaa?
JWTZ ni jeshi lenye sifa kibao za kushinda operations mbalimbali na nidhamu ipo pale, sasa ni wakati hawa jamaa wakawa front kwenye hii vita!JPM tusaidie..