Wazo : Nataka kutangaza harusi yangu feki nipate mtaji niingie shambani nikalime

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Wakuu , weekend imekaaje ?

Nimepata wazo fulani.

Sijawahi kufunga ndoa ila naishi na mwanamke kwa makubaliano fulani.

Kutokana na ugumu wa kupata mtaji wa fedha kwa ajili ya kuanzisha biashara hasa kujiingiza kwenye kilimo cha umwagiliaji , nimeamua nitengeneze harusi feki then mwisho wa siku michango ikishakamilika naahirisha harusi kwa sababu kwamba tumepishana / tumegombana na mwanamke wangu , na nitamtoa home aende huko kwao kwa muda.

Fedha ambayo itakuwa imechangwa nitakaa na Mwenyekiti na Mweka Hazina tujue cha kufanya , wachangiaji wataambiwa sherehe imesogezwa mbele wataarifiwa.

Nataka kuingia shambani.Yaani ninunue shamba la ekari 5 karibu na maji ya mto then nilime.Najua michango haitapungua 15mil.

Sidhani kama huu ni wizi , bali ni akili au wazo linalojenga.

Nikishafanikiwa kwenye kilimo ntafunga ndoa kwa gharama zangu na kuwaalika wale wote ambao walinichangia. Ili wasione kama pesa yao imeenda bure.

Ni kipindi cha ndani ya mwaka mmoja tu.
 
Braza ishu ni wachangaji.

Una uhakika mates wako wana uwezo wa kuchangia 30/30 mpaka 50??
 
Unafanya hata sherehe ya kimagumashi ya 3.5m ili kuzuga na kushusha mori zao hao machalii
 
Wazo hilo hilo likifeli, tangaza umekufa. tuchange rambi rambi, mchango ukitimia amka na kuwambia umerudi kwa msamaha wa malaika
 
Hili wazo liliwahi nijia hata mimi ila njaa ya kisenge sana 🤣🤣🤣...

Kuna mwana hapa kijiwe baada ya kimya cha muda ameropoka kitu nmecheka kinoma..nanukuu,,,

"Hivi nani aliyegundua mfumo wa kutumia pesa? amefeli sana, bora tungebaki na bater trade tu!"
 
Hili wazo liliwahi nijia hata mimi ila njaa ya kisenge sana ...

Kuna mwana hapa kijiwe baada ya kimya cha muda ameropoka kitu nmecheka kinoma..nanukuu,,,"ila aliyegundua mfumo wa kutumia pesa amefeli sana, bora
 
Kwa habari za Hivi punde utafeli kwenye hilo wazo lako. Ili ufaulu fanya haya:
Andaa mke feki, wakwe feki, wazazi feki, marafiki feki, na kanisa au msikiti feki wa kuitangaza hiyo ndoa halafu kwenye kamati uwe mwekahazina maaana hela yetu ya mchango tunaipigia bajeti na kuigawa sisi wenyewe. Wewe wala haikuhusu. Labda utumie hela ya Zawadi.
 
Back
Top Bottom