WAZO LANGU

Alpha M

Senior Member
Nov 8, 2016
165
156
MABADILIKO YA RATIBA UTOAJI WA HUDUMA ZA SERIKALI NA MASHINA YAKE KUANZIA 7:00AM HADI 3:00PM
Binafsi ninaamini anayeamka mapema zaidi ya mwenzake anayo nafasi kubwa ya kufanikiwa zaidi ya mwenzake (ikiwa wapo ngazi moja na wanafanya kazi masaa yanayolingana). Pia kwa wastani nchi nyingi zilizoendelea watu huamka mapema (pamoja na masaa mengi ya kazi) zaidi ukilinganisha na zile ambazo hajijaendelea. (Accrording to UNESCO)

Kila nchi inao mtizamo wake wa kazi pia utendaji wa kazi husika. Ratiba ya shughuli za kila siku hutofautiana kwa jamii moja na nyingine. Wafanya biashara wengi waliofanikiwa huamka mapema sana kabla hata ya 5:30AM na kufanya shughuli binafsi, baadae hao hao utawakuta ofisi za serikali kabla ya saa 8:00AM wanasubili huduma wakilalamika uchelewaji wa maofisa vitengo husika.

Maoni yako mwanajamvi wewe unamtizamo gani, je matokeo yatakua chanya au hasi kwa ujumla kwenye uzalishaji na utendaji wa wananchi na nchi kwa ujumla?
 
Back
Top Bottom