mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,286
- 6,727
Tangu Rais Magufuli ameingia madarakani, upinzani ubamkaba kooni kwa sababu kakataza kuendesha siasa, hasa mikutano ya hadhara ambayo wanadai wangeitumia kunadi sera zao. Sababu aliyoitoa Rais Magufuli ni kwamba anawajibika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama chake kuhusu maendeleo, hivyo kama ni kuendesha shughuli za siasa ziwe zinazohamasisha mageuzi ya kiuchumi.
Ukifuatilia kwa karibu, madai ya upinzani ni kuhusu kuminywa demokrasia, haki na uhuru, kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT), 1977, Sura ya Kwanza (Jamhuri ya Muungano, Vyama vya Siasa, Watu na Siasa ya Ujamaa na Jujitegemea), Sehemu ya Tatu (Haki na Wajibu Muhimu), hasa Ibara ya 18(1).
Tafiti za wachambuzi wa siasa, zimebainisha kuwa katika Dunia ya Tatu uongozi imara wa kisiasa unaweza kuwa mzuri au mbaya kwa maendeleo ya kiuchumi, kulingana na mambo makuu mawili. Kwamba matokeo ya uongozi imara wa kisiasa unategemea:
i) Mazingira ya nchi husika na hasa katika miaka ya mwanzo ya uhamasishaji mkubwa na ufuatiliaji wa mageuzi ya kiuchumi.
ii) Mitazamo ya wanasiasa na wananchi kwa ujumla, kuhusu siasa inaweza kuathiri, kwa kiasi kikubwa, juhudi za kiongozi wa kisiasa kutekeleza na kusimamia mageuzi ya kiuchumi, kama hana utashi wa kisiasa (Political Will) usioteteleka.
Isitoshe wachambuzi wa masuala ya kisiasa na maendeleo, wamebainisha kazi tatu za majukumu ya kiongozi thabiti wa kisiasa, ambazo ni mamlaka, kuhamasisha, na usimamizi.
Hoja ya msingi hapa ni kama Rais Magufuli ni mmoja wa viongozi ambaye ana kila sifa za uongozi imara wa kisiasa (strong political leadership) kwa maendeleo ya kiuchumi.
Kwa hoja hizo,
1) tuchambue na kuhukumu utendaji wa Rais Magufuli kulingana na jinsi uongozi wake unavyofanikiwa kusimamia mikakati yake kufikia malengo ya maendeleo ya kiuchumi.
2) Je, ni kweli madai ya viongozi wa upinzani kuwa Rais Magufuli ni dikteta ni sahihi? Kama ni sahihi, maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ya nchi yetu Tanzania, yanaathirika kwa kiasi gani?