(Unaweza isoma makala hii na nyingine nyingi za uwekezaji na ujasiriamali kwenye tovuti ifuatayo: Uwekezaji na Ujasiriamali )
ANGALIA UNAPENDA NINI KISHA KIGEUZE KUWA BIDHAA AU HUDUMA.
Kuna idadi kubwa ya watu ambao wamepata mawazo ya kuanzisha biashara kupitia njia hii na hatimaye kujitengenezea kipato kizuri. Kila mwanadamu kuna jambo fulani au kitu fulani ambacho yeye anapenda kufanya hivyo ni vyema ukajichunguza unapenda nini na hatimaye kugeuza hicho unachopenda kuwa bidhaa au huduma.
Mfano I
Kama wewe unapenda shughuli za kilimo unaweza kuanzisha shughuli za kilimo biashara (Agribusiness) ukijikita katika uzalishaji wa mazao ya biashara, pia waweza kuanzisha kiwanda cha usindikaji wa mazao ya kilimo ili kuongeza thamani na kisha kijitengenezea kipato kizuri kabisa.
Mfano II
Kama wewe unapenda maswala ya mitindo na urembo waweza kuanzisha kampuni itakayokuwa inashughulika na utengenezaji wa nguo ,vipodozi usambazi marashi ,mafuta ya kujipaka na bidhaa nyingine zinazohusika na mitindo na urembo.Unaweza kuanzisha saluni za kiume na za kike ilikuweza kufanya jambo unalolipenda na pia kujitengenezea kipato.
Mfano III
Kama wewe unapenda kusafiri unaweza kuanzisha kampuni itakayokuwa inatoa huduma za usafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine wakati ukijipanga kutanua wigo mpaka kutoa huduma za usafiri kimataifa.Waweza kuanzisha kampuni itakayokuwa inatoa huduma za usafiri katika sherehe mbalimbali kama harusi au kuingia mikataba na taasisi ambazo hazina magari ya kutosha hivyo kutoa huduma hiyo kwao na wakati ukijiingizia kipato.
Mfano IV
Kama unapenda tasnia ya teknolojia ya habari hii inaweza kuwa njia nzuri ya kuanzisha kampuni ambayo itajikita katika uandaji wa vipindi vya redio na televisheni pia unaweza kuanzisha kituo cha kurusha matangazo kwa njia ya redio au televisheni.Unaweza kuanzisha studio ya kurekodia matangazo ya biashara na kisha kuingia mikataba na makapuni au taasisi ambazo utakuwa unawaandalia matangazo yao ya biashara,pia unaweza kuanzisha huduma ya uandaaji wa makala mbalimbali wakati unafurahia kufanya unachopenda pia utakuwa unajitengeneza kipato kizuri .
Mfano V
Kama wewe unapenda maswala ya ufugaji kama kuku,ng'ombe ,mbuzi ,njiwa ,ufugaji wa samaki unaweza kuanzisha ufagaji biashara. Kwa hiyo utafuga mifugo kwasababu unapenda kufuga na wakati huohuo utakuwa unajitengenezea kipato .
Mfano VI
Kama wewe unapenda maswala ya uandishi na usomaji wa vitabu ,majarida unaweza kuanzisha kampuni ya kuchapisha (Publication Company)ambayo itajikita katika uchapishaji wa vitabu,majarida ,tisheti na vipeperushi hivyo kujitengenezea kipato.
Faida za njia hii
Tafiti zinaonyesha watu wengi wanaofanya kazi wanazozipenda huwa wanafanya kazi katika ufanisi wa hali ya juu.Mtu ambaye anafanya kazi anayoipenda ni mtu ambaye huwa na furaha maisha mwake, pia utakuwa unajitengenezea kipato kizuri hivyo utakapo amua kutumia njia hii kupata wazo la biashara utapata faida hizo nilizozitaja hapo juu.
Changamoto na suluhu yake.
Ushindani ndio changamoto kubwa katika njia hii hivyo unahitaji kuja na ubunifu wa hali ya juu ilikutoa huduma nzuri kulingana na ushindani ulioko sokoni; kwasababu unaweza kuta kitu unachopenda kuna mtu mwingine anakipenda pia na tayari ameshaanza kutoa huduma au bidhaa hiyo sokoni.Ukitaka kufanikiwa katika njia hii unatakiwa kutoa bidhaa nzuri na zatofauti na yule mshindani wako ilikuweza kupata wateja wakutosha.
Ushauri
Kabla ya kuanzisha biashara husika kupitia njia hii ni vema ukafanya tafiti za kutosha kuhusu soko la hiyo biashara unayotakakufanya na kisha kujua kama unachopenda kina weza kuwa bidhaa au huduma inayohitajika sokoni.Nakushauri ndugu yangu usikimbilie kuanzisha biashara bila kuwa na taarifa sahihi juu ya soko husika kwasababu mfanyabiashara huzalisha bidhaa zake kwaajili ya kuuza sokoni na si vinginevyo.
Itaendelea sehemu ya III
Imeandaliwa na James Albert.