Wazo kwa waziri wa madini

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,869
Reaction score
5,170
Mzee Jumanne Ngoma mvumbuzi wa madini ya Tanzanite mwaka 1967 mwili wake unaagwa kesho dar.
Madini haya hayapo popote duniani ni Tanzania.
Nashauri ili kuenzi jina lake pamoja na kwamba mgodi uko Mererani lakini mgodi upewe jina lake Ngoma Tanzanite mining.
Tusikubali kuzidiwa speed kama tulivyozungukwa na wazungu ziwa letu Nyanza eti kaja mjuaji mmoja anaitwa Speke kasimama pale keep left ya kwenda airport Mwanza kasema amegundua ziwa wakati lilikuwepo akaliita Victoria hii haikubaliki.
Mshauri mkuu wa nchi hata leo ameshauri daraja la dar liitwe Tanzanite.
Tujivunie chetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…