Waziri wa zamani wa Israeli akiri kutumiwa na Iran kuipeleleza nchi yake


SECRET AGENT

SECRET AGENT

Member
Joined
Jan 4, 2019
Messages
28
Likes
27
Points
15
SECRET AGENT

SECRET AGENT

Member
Joined Jan 4, 2019
28 27 15
9 Januari 2019
BBC SWAHILI

Waziri wa zamani wa Israeli, Gonen Segev anakabiliwa na kifungo cha miaka 11 jela baada ya kukiri kuchukuwa taarifa za nchi yake na kuzipeleka Iran, wizara ya ya sheria ya Israel imesema.

Segev, ambaye alihudumu kama waziri wa nishati miaka ya 90 inasemekana alianza kufanya shughuli hiyo wakati akiwa daktari nchini Nigeria.

Alituhumiwa kwa kuvujisha taarifa za maafisa wa Israeli na sehemu za usalama.


Segev alikamatwa na kuwekwa kizuizini Guinea ya Ikweta mwezi Mei 2018 na kusafirishwa kwenda Israeli. Amekiri makosa ya kuhusika na matukio makubwa ya ujasusi kama sehemu ya makubaliano yake na waendesha mashitaka ili apunguziwe adhabu.

Sagey mwenye miaka 63 atasomewa hukumu Februari 11.

Mamlaka za Iran hazijazungumzia lolote kuhusu kesi hiyo mpaka sasa.

Tangu mapinduzi ya mwaka 1979, ambapo viongozi wenye msimamo mkali walishika hatamu za uongozi wa Iran wamekuwa wakitishia kufutwa kwa taifa la Israeli.

Iran inapinga uwepo wa Israeli ikisema kuwataifa hilo halina uhalali wa kuwepo kwa kuwi wamechukua ardhi ya Waislamu.

Mwaka 2005, Sagey alihukumiwa miaka mitano jela baada kukamatwa akisafirisha tembe 30,000 za dawa kutoka Uholanzi kwenda Israeli huku akitumia kibali cha kusafiria cha kidiplomasia ambacho kimekwisha muda wake.

Pia alinyanganywa leseni ya kufanya shughuli za afya, lakini aliruhusiwa kufanya kazi kama daktari akiwa Nigeria ambapo alihamia baada ya kutoka jela 2007.

Afisa wa usalama wa Israeli Shin Bet, amesema mwezi Juni Sagey alikiri kuwasiliana na maafisa wa ubalozi wa Iran akiwa Nigeria mwaka 2012 na alitembelea Iran mara mbili kukutana na muhusika aliyekuwa anawasiliana nae.

Inasemekana huko alikuwa akitoa taarifa zinazohusiana na sekta ya nishati, vituo vya usalama Israeli na taarifa za maafisa wa kisiasa na taasisi za ulinzi.

Taarifa zaidi kuhusiana na kesi hiyo zimebaki chini ya maafisa wa usalama.

"Ofisi ya waendesha mashitaka ya wilaya inataka kutoa taarifa zaidi kuhusiana na uhusiano huo na zikitoka itaeleweka wazi kwamba Segevni kweli alikua akiwasiliana na Iran lakini si kwaajili ya kuwasaidia," timu ya mawakili ya Segev imeliambia gazeti la Yedioth Ahronoth.Sent using Jamii Forums mobile app
 
moto wa maji

moto wa maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2016
Messages
3,595
Likes
2,045
Points
280
moto wa maji

moto wa maji

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2016
3,595 2,045 280
Mbinu ya kizamani sana hiyo ,Israel badilisheni mbinu acheni hiyo
 
chisluk

chisluk

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2016
Messages
253
Likes
152
Points
60
chisluk

chisluk

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2016
253 152 60
israel haiwezi kufutwa kwenye raman ya dunia na taifa lolote lile
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,124
Likes
10,783
Points
280
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,124 10,783 280
israel haiwezi kufutwa kwenye raman ya dunia na taifa lolote lile
Nani kasema?? Mbona Hitler aliweza? na kma sio uingereza kuingilia kungekuwa hakuna muisraeli hii dunia......

Dunia hii kulikuwa na mataifa makubwa sana ila leo hii yamefutwa kwenye ramani ilikuwepo Ottoman empire ilikuwepo Mongolian empire achilia Austrian empire zilizokuwa zina mamilion ya watu ila zilisambaratishwa ndio sembuse hako kataifa kma wilaya ya Temeke wanakokalia kimabavu ndio kasifutwe??

Mahaba ya kidini yanatuangamiza watu weusi
 
Ndumbula Ndema

Ndumbula Ndema

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Messages
4,512
Likes
3,575
Points
280
Age
51
Ndumbula Ndema

Ndumbula Ndema

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2018
4,512 3,575 280
Huyo ndo basi tena
 

Forum statistics

Threads 1,250,884
Members 481,523
Posts 29,749,538