kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,870
- 7,752
Wananchi tunaofuatilia kipingi cha live maswali na majibu bungeni hakika waziri wa viwanda, Charles Mwijage amekuwa anatuangusha kwa kutokidhi kiu ya wasikilizaji/watazamaji wake kwa majibu hafifu yasiyoridhisha.
Huyu inaelekea anajali zaidi kuonyesha mbwembwe na mikogo kuliko kile anachokieleza. Pia inaonyesha kiitikadi hayuko kwenye mstari wa mkakati wa serikali ya CCM kwani ameonekana mara kwa mara akitupia lawama sera na sheria kama vitu vinavyomkwaza kufanya maamuzi. Badala yake inaoonekana angependelea uhuru kufanya anavyoona yeye kitu ambacho kinaweza kusababisha matumizi mabaya ya madaraka.
Hata hivyo nachopenda kumshauri Waziri Mwijage kama hana majibu sahihi basi awe anafanya homework yake kama waziri kisha awe mtulivu anapojibu maswali kwani enzi za ubabaishaji zimepita.