Waziri wa fedha fanyia kazi pendekezo la aliekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini,David Kafulila

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,325
152,136
Mara kwa mara,ndani ya Bunge na nje ya Bunge, aliekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini,mh.David Kafulila, alikuwa akipendekeza na kusisitiza kuwa makampuni ya kuchimba madini, makampuni ya simu n.k yanatakiwa yasajiliwe katika Soko la Hisa la Dar-es-salaam (Dar-es-salaam Stock Exchange) kwa lengo la kuhakikisha makampuni makubwa haya hayakwepi kodi na pia yanalipa kodi sahihi serikalini.

Mh.Waziri,kwasababu serikali hii imeamua kulivalia njuga swala la ulipakaji kodi,basi nakushauri ulifanyie kazi wazo hili la kijana mzalendo wa nchi hii,ndugu David Kafulila ili kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya serikali sambamba na kudhibiti ukwepaji wa makampuni makubwa katika ulipaji kodi.

Nawasilisha.
 
Last edited by a moderator:
H

Cha msingi hapa ni hoja ya Kafulila na wala si Kafulila kama mtu binafsi.

Huwezi kumtofautisha mtoa hoja na hoja yake kwa sababu, hakina kichwa cha serikali ambacho kila mtu anaweza kwenda kuchota maarifa na kuyawasilisha.

Nimeona hiki kitu kimekuwa kawaida kwa marehemu ccm, kuendelea kuimba nyimbo, UKaWA hivi ukawa vile wakati hakuna kitu wanachoweza kufanya bila mchango wa ukawa. Kila kitu wanaiba UKAWA na wanatambua UKAWA ni dunia nyingine na ndiyo sababu wanaogopa UKAWA kuliko Ebola.

Kwa mantiki hiyo, Kafulila anafanana na hoja zake, kama vile Lusinde, Mulugo, Jk, Makamba, Ndasa n,k wanavyofanana na vichwa vyao!.
 
Mtoa post...kabla ya Kafulila hukuwahi kusikia kuhusu makampuni binafsi kuobwa kujiandikisha kwenye soko la hisa? Najua umewahi...Hivyo hii hoja sio ya Kafulila....Wengi tu wamewahi kusema kuhusu hili kabla hata ya kuundwa kwa DSE mwaka 1996.

Jambo lingine...kuna vigezo vya makampuni ku-go public....na hayapaswi kulazimishwa. Ikiwa ni swala la kulipa kodi...serikali isimamie tu sheria zilizopo na wala sio lazima mpaka kampuni ziandikishwe DSE ili kufanya serikali ipanue wigo wake wa mapato. Sio lazima kabisa.
 
Nimeshukuru nulijua tu atakimbia
 
Kwakuwa ccm imechokwa,
Na kwakuwa ili kurudusha imani kwa wananchi ccm inaiba Sera za ukawa,
Na kwakuwa Kafulila ni mmoja wa wanaUKAWA,
Basi naunga mkono mawazo ya mtoa mada.
 
Back
Top Bottom