Waziri Ndalichako, bila kuelewa baada ya hilo la divisheni na GPA utaibuka na nini, sielewi ni kwa jinsi gani utafanyakazi na Naibu katibu mkuu wako anayeshughulikia elimu ya juu. Yaonekana ameshindwa kabisa kuelewa kwamba sasa hivi ana nguvu ya utawala kwa elimu ya juu na watendaji wake. Badala yake anafanya urafiki na viongozi hao kama officemates wake.
Kwa sasa yuko katika juhudi za kukwamisha utatuzi wa matatizo ya uongozi yanayokikabili chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine. Hivi karibuni alitembelea chuo baada ya kuwasiliana na uongozi tu! Hapo Nyuma, Chama cha wanataaluma kilimwandikia barua waziri Ndalichako kikitaka aingilie kati matatizo ya upendeleo, wizi wa pesa za wastaafu, ufisadi, uduni wa majengo yaliyojengwa, watumishi kulipwa mishahara isiyostahili yao, chuo kuwa na watendaji wasioweza kutekeleza kazi zao, nk. Ktk barua hiyo ushahidi uliambatanishwa na kumuomba waziri afike kuzungumza na wanataaluma.
Naibu katibu huyu amelibeba na kuahidi kulishughulikia. Imekuwa ni ajabu kwamba badala ya kuyatatua, amefika chuoni na kuteta na viongozi ambao ndo watuhumiwa kwa uzembe na amegeuka baada ya kufanya party na vinywaji kedekede na viongozi hao. Anasema haoni kibaya. Hajaongea na wanataaluma, hajatembelea au kuuliza kwa walalamikaji juu ya matatizo hayo, amekukuwa sehemu ya utawala na sasa analeta vitisho kwa wanataaluma. Sijui kama anajua mipaka ya kazi zake au kama anaijua kasi ya utawala wa sasa.
Hata kama kapozwa kwa pesa kama tunavyosikia, huyu hastahili kuwa Naibu katibu mkuu wa wizara hii. Sijui uwezo wake wa huko alikotoka lakini kwa mwanzo huu sioni kama una msaidizi ktk kazi.
Waziri ingilia kati maana tunachokiona ni kuendeleza upuuzi katika uongozi.