Waziri wa Afya awasimamisha kazi watumishi NHIF

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,353
2,846
Watumishi kadhaa wa NHIF akiwemo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wamesimamishwa kazi na Waziri wa Afya Mh. ummy Mwalim kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha.

Habari kamili kuwaijua punde.

======================

nhif1.jpg

nhif2.jpg

Chanzo: Mediahuru
 
Jipu limehamia wizara ya Afya, Naibu mkurugenzi NHIF kasimamishwa.

Waziri Ummy Mwalimu amewasimamisha vigogo kadhaa wa NHIF kutokana na ubadhirifu wa pesa za umma.
 
mtoa taarifa hebu andika kisomi tuelewe...tuna ndugu zetu huko NHIF..
 
Sasa mkuu ni vigogo kadhaa au naibu mkurugenzi?weka vizuri nina jirani yangu huko NHIF ana mbwembwe sana mtaani.
 
Waziri U. Mwalimu awasimamisha kazi maofisa wakuu 4 wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa tuhuma za wizi wa zaidi ya Sh2bn katika akaunti ya NHIF Mara.

VIGOGO WALIOSIMAMISHWA NHIF: Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Michael Mhando, Mkurugenzi wa Fedha, D. Rutazaa, Mkurugenzi wa Habari, A. Othman na Mkaguzi Mkuu, A. Maneno
 
Ni habari tuazozitarajia kila kukicha, ila isiishie kuwasimamisha kazi tuhuma zikithibitika wafikishwe mahakamani.
 
Habari imeletwa kienyeji kabsa..!sijui ata tuanzie wapi?zaidi ya kuuliza maswali mengi tuuh..!
 
NHIF kuna madudu mengi sana! CAG anatakiwa akafanye special audit haraka! Kuna madudu mengi sana hasa kwenye kulipa pharmacy kubwa kubwa na hospitali binafsi_Wamechomekea sana cha juu na kwenda kuchukua mlango wa nyuma! Inajulikana wazi kabisa!
 
Nilitegemea kitu kama hiki bado NHC na NIC
Hii nchi ilikuwa imeoza kwa ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma. Kila mtu alikuwa anakomba kama hana akili nzuri. Kikwete yeye alikuwa kazi yake ni kucheka tu. Sijawahi kuona rais bogas namna hii dunia yote. Magufuli ana kazi kubwa sana kwani anadeal na uozo uliotanda kila kona.
 
Aongeze nguvu kidogo majipu yapo mengi sana
 
Mimi hadi sasa sijui ni jinsi gani naweza kujiunga na huu mfuko. Sijaajiriwa nafanya shughuli zangu binafsi. Ila NHIF hawaelimishi watu jinsi ya kujiunga.
 
Jipu limehamia wizara ya Afya, Naibu mkurugenzi NHIF kasimamishwa.

Waziri Ummy Mwalimu amewasimamisha vigogo kadhaa wa NHIF kutokana na ubadhirifu wa pesa za umma.
bima ya afya kila siku kusimamishwa, kaimu mkurugenzi aliyekuwepo alisimamishwa , huyu kaimu naye kasimamishwa dah
 
Back
Top Bottom