barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Bado kipindupindu kimeendelea kuwa tishio katika Jiji la Dsm na viunga vyake,makambi ya watu walioathirika na kipindupindu yanaendelea kupokea watu siku baada ya siku,hata kama haitangazwi kwa "nguvu" kuficha aibu hii,lkn bado watu wanapoteza maisha sbb ya uchafu na kula kinyesi.Wanasema ili mtu aweze kupata kipindupindu basi ni lazima awe amekula wastani wa vijiko sita vya kinyesi vyenye ujazo wa kijiko cha chai.Ndio kusema kipindupindu ni matokeo ya kula na kuramba kinyesi chenye uwingi wa vijiko sita.Huu ni ugonjwa wa aibu sana.Ukienda Ukerewe,ukija Geita mpaka Pawaga Iringa na kaskazini ya Arusha na Moshi,ugonjwa huu wa aibu wa kula kinyesi umeshamiri.
Tamko kali la Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,ilikuwa ni kuzuia uuzaji na ulaji wa matunda yaliyowazi.Mama Ntilie waliimizwa kuuza vyakula vya moto na vilivyo ktk mazingira safi,wauza matunda wake kwa waume walihimizwa kuuza matunda yasiyomenywa ili kuepuka mrundikano wa inzi na vimelea vya magonjwa.Baada ya agizo hilo,tulimuona mkuu wa Wilaya ya Kinondoni bwana Makonda na yule wa Temeke Miss Temba,wakiimiza usafi wa jiji na kuzuia katukatu watu kuuza matunda yaliyomenywa na kuachwa wazi.Mabwana afya wa Wilaya za jijini Dar walianza na nguvu za "soda" kwa kufuatilia hilo ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku maji ya kwenye mifuko maarufu kama "maji ya Kandoro"
Ummy Mwalimu,hata baada ya katazo hilo,bado matunda yaliyomenywa na yasiyo na uwngalizi wowote wa kiafya yameendelea kuuzwa ktk jiji la Dsm,na mbaya zaidi hata nje karibu ya ofisi za Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.Swali la kujiuliza,Je katazo hilo lilikuwa nguvu ya soda na "attention" ya media??kuna mkakati gani endelevu kuhakikisha tabia hii ya kuuza vyakula ktk mazingira yasiyo rafiki kwa afya inakoma?Kwa sasa ni msimu wa mananasi ya kutoka Msoga kwa mstaafu wetu,mengi yamepangwa barabarani na yanauzwa yakiwa yamemenywa bila hata kufunikwa,je kipindupindu huu sio ndio mwanzo wake?
Waziri Ummy Mwalimu na wasaidizi wako,tunaomba msimamie katazo hili,isiwe ni nguvu ya soda na kutoa matamko mbele ya vyombo vya habari,bali uwe ni utekelezaji wa dhamira ya kweli wenye msukumo wa utumishi wa kweli kwa wananchi.
Wabilakh Tawufiq
Ndimi barafu