Waziri Ummy Mwalimu: Marufuku RC, DC kuwakamata na kuwasumbua madaktari

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,863
Katika kuelekea siku ya Wanawake Duniani,Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,amepiga marufuku wakuu wa mikoa na Wilaya (RC and DC) kuwadhalilisha kwa kuwasweka lupango au kuwasumbua madaktari ktk mikoa na Wilaya zao.

Waziri Ummy anasema kwa sasa imekuwa kama "fashion" kwa RCs na DCs kuwakamata watumishi wa umma na hasa madaktari na kuwaweka ndani bila sababu zenye mashiko,kiasi kwamba imeshusha morali ya kazi kwa watumishi hao wa afya au wale walio chini yao.

Mh.Ummy anasema jukumu hilo si lao kisheria,hivyo wanapaswa kuliacha mara moja,waziri amesisitiza kuwa ameshakubalina na Waziri wa TAMISEMI kuwaelekeza wakuu wa Wilaya na Mkoa mipaka yao ya kazi ili wasiingilie kazi na taratibu zilizo nje ya majukumu yao.

Yeye kama Waziri wa Afya,hakuwa tayari kuona madaktari wakinyanyaswa na kusumbuliwa na Wakuu wa mikoa na Wilaya bila sababu.

Agizo hili limekuja siku chache baada ya mkuu wa mkoa wa Singida Dr Nchimbi kumuweka ndani DMO wa Singida,kitu kilichosababisha Daktari huyo kuandika barua ya kujiuzulu na kuacha kazi.

Huko Arusha,RC Gambo hivi karibuni,alionekana ktk vyombo vya habari akimfokea na kumshutumu Daktari kwa makosa ambayo sio yake moja kwa moja.
image.jpeg

Huko Lindi,Wilaya ya Kilwa,DC wa Wilaya hiyo,Mh.Ngubiagayi alimdhalilisha Daktari mbele ya vyombo vya habari kwa kuamuru polisi wamshikirie kwa kosa asilohusika nalo moja kwa moja,kitu kilichosababisha chama cha Madaktari Tz,kuweka katazo la kupewa ushirikiano kwa kiongozi huyo popote pale Tz.

Kwa kauli hii ya Waziri mwenye dhamana,akishirikiana na Waziri wa TAMISEMI,bila shaka wakuu wa Mikoa na Wilaya,watajua mipaka yao na kuheshimu taaluma za watu na kufuata misingi ya kanuni,sheria na taratibu na si kukurupuka mbele ya kamera ili waonekane kwenye TV.
 
Hao maRC na maDC waliteuliwa kwa kigezo cha urafiki na kulipana fadhila.Raia wakinung'unika kuhusu uteuzi wa kulipana fadhila kichama wanaonekana wapumbavu......Bakini na ubashite wenu kama mtu ni faktari na ana profesional yake anaweza akaajiliwa kwenye hospital za binafsi, akajiajiri au akaajiliwa hata nje ya nchi.
 
utawala huu wa mfalme mtukufu hauna coordination, wengi wa hao maDC na maRC ni coppies za mtukufu kwa mambo wafanyayo ila amshangae yule msaidizi wake kutwa kufukuzana na mapunga mtandaoni
Katika kuelekea siku ya Wanawake Duniani,Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,amepiga marufuku wakuu wa mikoa na Wilaya (RC and DC) kuwadhalilisha kwa kuwasweka lupango au kuwasumbua madaktari ktk mikoa na Wilaya zao.

Waziri Ummy anasema kwa sasa imekuwa kama "fashion" kwa RCs na DCs kuwakamata watumishi wa umma na hasa madaktari na kuwaweka ndani bila sababu zenye mashiko,kiasi kwamba imeshusha morali ya kazi kwa watumishi hao wa afya au wale walio chini yao.

Mh.Ummy anasema jukumu hilo si lao kisheria,hivyo wanapaswa kuliacha mara moja,waziri amesisitiza kuwa ameshakubalina na Waziri wa TAMISEMI kuwaelekeza wakuu wa Wilaya na Mkoa mipaka yao ya kazi ili wasiingilie kazi na taratibu zilizo nje ya majukumu yao.

Yeye kama Waziri wa Afya,hakuwa tayari kuona madaktari wakinyanyaswa na kusumbuliwa na Wakuu wa mikoa na Wilaya bila sababu.

Agizo hili limekuja siku chache baada ya mkuu wa mkoa wa Singida Dr Nchimbi kumuweka ndani DMO wa Singida,kitu kilichosababisha Daktari huyo kuandika barua ya kujiuzulu na kuacha kazi.

Huko Arusha,RC Gambo hivi karibuni,alionekana ktk vyombo vya habari akimfokea na kumshutumu Daktari kwa makosa ambayo sio yake moja kwa moja.View attachment 477904

Huko Lindi,Wilaya ya Kilwa,DC wa Wilaya hiyo,Mh.Ngubiagayi alimdhalilisha Daktari mbele ya vyombo vya habari kwa kuamuru polisi wamshikirie kwa kosa asilohusika nalo moja kwa moja,kitu kilichosababisha chama cha Madaktari Tz,kuweka katazo la kupewa ushirikiano kwa kiongozi huyo popote pale Tz.

Kwa kauli hii ya Waziri mwenye dhamana,akishirikiana na Waziri wa TAMISEMI,bila shaka wakuu wa Mikoa na Wilaya,watajua mipaka yao na kuheshimu taaluma za watu na kufuata misingi ya kanuni,sheria na taratibu na si kukurupuka mbele ya kamera ili waonekane kwenye TV.
 
Waziri hajui kama hao ma DC na RC ni wawakirishi wa Raisi Moja kwa moja?? Tamko lake linaidhalilisha Taasisi ya Uraisi moja kwa moja... alafu ndio zake kumpinga raisi one day Raisi alitangaza kufyatua watoto yeye akaja na Tangazo lake kuwa Raisi alikuwa anatania! wakati ni ukweli Watoto watasomeshwa bure... Japo kauli ya majuzi ilisema bure isahaulike masikioni mmwetu! o_O
 
hakuna mtu anatakiwa awe free from stress kama dakitari anzia uchungu wa shule miaka 5 yote hakuna kupumzika wewe na Kitabu mwanzo mwisho halafu leo mtu anatokea tena kwa mambo ya kisiasa anasema uwekwe ndani bila sababu ya maana sidhani kama linaleta Maana, Ni haki ya kila mtumishi kufanya kazi kwa Amani
Tutenganishe Siasa na Utaalamu sio kila jambo linahitaji siasa ndani yake.

Hongera Waziri Ummy Mwalimu Najua unaelewa kazi kubwa madaktari wanayofanya.
 
Safi sana Mh waziri, umeokoa taaluma muhimu sana, nasubiri waziri wa elimu nae awasimamie walimu.
 
Sasa akili ya Bashite Mkuu na wakuu wake wa Mikoa na Wilaya ni jambo moja...Bashite Mkuu ndo anachopenda..

Na akili ya Ummy Mwlm, Simbachawene na akina Nape Nnauye ni jambo jengine...Bashite Mkuu anawasikiliza kina Mrisho Gambo, Daudi Bashite na Ally Salim Happiness kuliko Mawaziri wake!
 
Nilishamwambia dc mmoja rafiki yangu kimtindo ya kwamba hiyo style wanayotaka kutupeleka wakiongozwa na Bashite mkuu haitafanikiwa na hawataweza kamwe kwani sio rahisi watanzania wa leo na dunia ya leo wakakubali kupelekwa kikaburukaburu au kichinachina na hata ki~North Korea.
Katu aslan wasitarajie kufanikiwa ni suala la mda tu.
 
Back
Top Bottom