Waziri Ummy Mwalimu akemea na kuagiza kukamatwa kwa watu waliompiga daktari Mtwara

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemuagiza mkuu wa mkoa wa Mtwara kuhakikisha wananchi waliohusika na tukio la kupigwa kwa daktari wa hospitali ya rufani mkoa wa Mtwara, Ligula wanakamatwa.

Ndugu wa mgonjwa walijichukulia sheria mkononi na kuamua kumpiga daktari huyo baada ya ndugu yao mgonjwa kupewa rufaa ya matibabu kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili.
 
Kuchukua sheria mkononi si jambo jemba, hao wananchi wamefanya vibaya sana ni bora wakamatwe wakaelezee kilichotokea na sharia ifate mkondo na wakishakamatwa na wale madr. na manurse wanaoua wagonjwa kizembe nao wachukuliwe hatua za kisheria, wananchi sasa hivi hakuna kufunika kombe, Nurse au Dr. akifanya kosa kwa makusudi, tukashtaki polisi tufungue kesi mahakamani.
 
Si bure, labda kuna muongozo itakuwa wameupata hao wana kuchele kutoka kwa Second Master. Wakamatwe haraka.
 
Kuchukua sheria mkononi si jambo jemba, hao wananchi wamefanya vibaya sana ni bora wakamatwe wakaelezee kilichotokea na sharia ifate mkondo na wakishakamatwa na wale madr. na manurse wanaoua wagonjwa kizembe nao wachukuliwe hatua za kisheria, wananchi sasa hivi hakuna kufunika kombe, Nurse au Dr. akifanya kosa kwa makusudi, tukashtaki polisi tufungue kesi mahakamani.
NI KWELI KABISA,ILA MPAKA WAZIRI ANATOA TAMKO AKINA RPC WAPO WAPI?KIUKWELI WATU WANA MIHEMKO MIBAYA SANA,...HATA HILI NENO "HAPA KAZI TU"LINATUMIKA VIBAYA-"HAPA KAZI NA AKILI TU"....HAO WANANCHI WAKAMATWE NA UCHUNGUZI UFANYWE
 
Kuna mdau mmoja aliwahi kuniambia Wananchi wana kiburi sana. Ni rahisi tu kukuchonganisha na kiongozi wa kisiasa, na kwa kuwa ni mileage kisiasa basi utaambiwa anasimamishwa kazi kupisha uchunguzi. Yaani maneno ya upande mmoja tayari mtu unasimamishwa kazi tena kupisha uchunguzi tena wakati mwingine siyo rushwa au wizi bali tu hata fitina,ajabu sana.
 
Vyombo vya usalama vichukue hatua sitahili kwani hali hii ikiachwa wataalamu watakuwa hatarini
 
Ummy mwalimu anakurupuka naye kwanza wizara imemuelemea hawezi kitu.mambo ya ustawi Wa jamii n maendeleo ya jamii kayatupa kule Jana kuna taarifa za mjane arumeru kafanyiww kitendo cha kikatili n wanakijiji ambao hawajulikani ni bibi Wa miaka 85 hivi anawajukuu n mjane amekatiwa mazao yote shambani kwake n aliyekuwa anamtetea kajeuruhiwa na mapanga na kuchomewa gari lake hapo ustawi Wa jamii wako wapi?hiyo wizara imemlemea anakimbilia madaktari wakati issue hizi zinamshinda kuna changamoto nyingi sana za wizara kwanza nashindwa kuelewa ni kwanini wizara ilivunjwa.
 
kwangu nilitegemea na ninategemea mambo kama haya yajitokeze kwa wingi,kama hili la mtwara halitapewa adhabu kali kwa hao wananchi waliofanya hicho kitendo.kwangu naona viongoz wa kisiasa wamerudisha madaraka kwa wananchi na kupokonya maamuz kwa wataalamu/professionals.Leo hii daktari anasimamishwa na media kuitwa just kwa hearsays,kila politicians anatumia media kwa advantage yake,mwisho wa siku raia wanawadharau wafanyakazi na kuwachukia bila kujua wao ndio watakao umia
 
Si Ndio Mlilokuwa Mkilifanya Ninyi Kuwadharirisha Wataalam Hao!!? Mlidhani Ndio Njia Pekee Iliyo Sahihi!!! Sasa Wananchi Wanaendelea Pale Ambapo Mmeishia Ninyi!!!
 
Back
Top Bottom