Waziri Prof. Ndalichako alimsahau RC Makonda au alimaanisha nini

Wakati wa ufunguzi wa mabweni mapya ya UDSM wakati wa hotuba yake hakutambua uwepo wa RC Makonda, badala yake aliwatambua wengine na wakuu wa wilaya tu. Hii ilikuwa bahati mbaya au kuna jaambo?

Ni ishara kwetu tunaolalamika kuhusu ' Qualifications ' za Makonda Bashite kwamba tayari ameshathibitisha pasipo na chembe ya shaka kuwa hastahili kuwa Mkuu wa Mkoa hivyo kumtambua pale mbele ya ile ' hadhara ' pengine ' Uprofesa ' wake ungeingia ' doa '.

In short tu ni kwamba Mama Ndalichako kaamua ' kujilipua ' huku akihanikizwa na ile kauli ya ' Kisela ' ya kama noma na iwe noma.....potelea mbali!
 
Ajiandae kutimuliwa.

Huyo Mama CV yake si ya ' sport sport ' Mkuu na kama unakumbuka hata wakati wa awamu ya nne ya Kikwete pia alishawahi kufukuzwa / kuondolewa nadhani katika Cheo cha Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania lakini unaambiwa bado ' Taasisi ' zingine zinazojitambua na kumtambua zikamwajiri hadi Rais wa Awamu ya Tano ( 5 ) Dkt. Magufuli alipomteua tena na safari hii kuwa full Minister wa Wizara anayoiongoza.

Sasa fukuzwa au furumushwa Wewe huko ulipo halafu uone kama utapata tena Kazi na sana sana utarudi zako tu kwenu huko Kijijini kuvuna ' mabua '.
 
Back
Top Bottom