Waziri Ndugulile aagiza tozo za usajili wa Blogs, online TV zishuke

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Waziri wa Mawasiliano na Tehama, Faustine Ndugulile ameitaka mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kuangalia upya tozo kwa ajili ya mitandao ya kijamii ili vijana waweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

Ameyasema hayo jijini Arusha wakati akiwa Katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha ya kutembelea taasisi za serikali zilizopo chini ya wizara yake na kuangalia namna wanavyofanya kazi ambapo alisema kuwa ni vyema mamlaka hiyo ikajikita zaidi kutoa Elimu kwa jamii kwani na ni kosa kisheria kutumia mtandao wa kijamii bila kusajiliwa.

Aliwataka TCRA kupunguza gharama za usajili wa mitandao ya kijamii ili vijana waweze kujiajiri kupitia mitandao hiyo ambapo alitoa muda wa mwezi mmoja kuhakikisha Sheria zote zimepitiwa na muda wa usajili wa mitandao hiyo umefunguliwa.

Alipoongeza TCRA kanda ya kaskazini kwa kutoa Elimu kwa mafundi simu na kusema kuwa elimu hiyo itawasidia mafundi hao kutambulika kisheria ambapo alizitaka kanda zingine kuiga mfano huo.

"Niwaonye mafundi simu wote wale ambao wanafuta IMEI namba za simu ambazo zimeibiwa na kuweka IMEI namba mpya waache mara moja kwani wizara ina mashine ambazo hata ukifuta simu inatambua ambapo alisema kuwa iwapo fundi yeyote atabainika amefanya uhalifu huo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake"amesema

Ndungulile aliwataka wananchi kufahamu kuwa ifikapo Juni 30 laini zote za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole zitafungiwa kwani serikali ilishatoa muda wa kutosha kwa kwa wananchi kusajili kwa alama za vidole.

Katika hatua nyingine waziri aliwataka wafanyakazi wa shirika la posta uongeza ubunifu zaidi pamoja na kuongeza ufanisi Katika utendaji wao wa kazi ,huku akiwataka watumishi wa posta ambao hawajui komputa kwenda kujifunza kwani iwapo huduma za posta kwa njia ya namba yako ya simu ikianza (virtual box )mfanyakazi ambaye hajui kinakilishi hawatakuwa na kazi.

Alitaka wizara yake kuarakisha mabadiliko ya sheria, ikiwemo mabadiliko ya sera ya posta ambapo pia aliwataka mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kusimamia sheria ya usafirishaji ,huku akiwasisitiza majukumu ya posta yalindwe ila kwenye kazi wakafanye kazi vyema bila kuingiliana.

Kwa upande wake meneja wa Kanda ya kaskazini wa mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Mhandisi Emelda Salumu alisema kuwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania kwa upande wa Kanda ya kaskazini kwa mwaka wa fedha 2020 /2021 wanampango wa kukusanya kiasi cha shilingi billioni moja millioni 27 ambapo hadi sasa wamekusanya kiasi cha shilingi millioni mianane na kumi na nne thelasini nane

Alisema katika kuhakikisha uhalifu kupitia mitandao ya simu unapungua wameamua kutoa elimu kwa wananchi pamoja na mafundi simu ambapo mafunzo 332 wamepatiwa kwa upande wa Kanda ya kaskazini ambapo kwa upande wa Kilimanjaro mafunzo 67 wamepewa, Arusha 133 Tanga 67 na Manyara 78 ambapo kwa Manyara bado wapi kwenye mafunzo.

Alisema mafunzo haya yatawasaidia kuwa wafanisi Katika kazi zao pia wataona utofauti yao waliopewa mafunzo pamoja na wale ambao hawakupewa mafunzo.

Ends...
 
Back
Top Bottom