Waziri Nchimbi ahamsisha wabunge wajiunge na mitandao kama JamiiForums

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
989
Alikuwa akihitimisha hoja za wabunge kuhusu Bajeti yale masaa sita yaliyopita.

Alifika mahala siku hizi taarifa za meseji za simu ni nyingi kuliko maelezo na yeye kama Waziri na hata IGP wanazipata na wanazijadili na wakati mwingine wanazifanyia kazi.

Kisha akawasihi wabunge kwamba tembeeleeni mitandao ya kijamii muone vijana wetu wanavyojibizana huko....

MY TAKE:

Kwa kauli hii, basi hata waliokuwa wanchukia hii kitu iitwayo Jamii Forum, forum inayoongoza kufumua chochote toka kokote kiliko basi tutarajie ID mpya nyingi kuanzia sasa na wenye ujasiri watajitokeza waziwazi kama tulivyojulishwa ujio wa Mama Tibaijuka wiki mbili zilizopita.
 
Wache waje tu,kama wanakuja na point tuta wajibu kwa points,na kama wanaleta ukilaza wao vile vile tuta deal nao hamna kuwaacha wajinga wanao kuja kuharibu thread...tunawakaribisha

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Wakuu, Nchimbi kweli hajui ya kuwa wabunge walio wengi ni members wa social network? Mie nafikiri angetumia busara kuwashauri wawe verified users kuliko kuendelea kutumia fake ID. Wasi wasi wangu ni endapo watakubali kuwa verified kwani wengi wao hawana uwezo wa kujenga hoja.
 
Angeanza yeye kuja hapa awe verified user tumhoji hapa kwenye hili bunge la Dunia siyo anapita huku kama Jambazi then anaenda kwenye lile Bunge lao kutetea Jangili.
 
Lingekua jambo la busara sana kama wangekuwepo lakini naona kama vile wazushi tu and cowards (social worries are not their concerns at heart), yule mama waziri alikuja hapa akasema apewe maswali atayajibu mpaka leo ajatokea tena baruti. Sijui ndio alitaka tumuone mtu wa watu ama vipi mi hata sielewi.
 
hakuna chanzo kikuu cha habari kama jf, hao wabunge wa ccm waambiwe hapa hakuna kugonga meza ni hoja tu.
 
TehTeh, Mimi mbona nipo siku nyingi na ni Waziri wa JK!
Acha ukunguru. Unaogopa nini kujitambulisha kama kweli wewe ni waziri wa sirikali iliyoshindwa kazi? Serikali ya jk ni janga yawezekana unahofu kupopolewa mawe ukijulikana. Au wewe ni Mlugo, aka.... Kazi. ipooo.
 
serukamba asije hatutaki matusi, aende aungane na kundi la wahuni wenzie kina nape, kinana, mwigulu na lusinde wako na group yao facebook

Serukamba ndo mimi,nmeishi sana marekani lile neno USA sio tusi,sema nyie wabongo hamna dogo!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
TehTeh, Mimi mbona nipo siku nyingi na ni Waziri wa JK!

kama kweli ni waziri, ndo maana kazi haziendi coz kila wakati nakuona ukiwa jukwaa la wakubwa ukipost picha za mademu. Kwa mtindo huu kazi haziwezi kwenda kama unshinda kupiga picha videmu
 
Wanaoafiki waseme ndiyo, wasioafiki waseme hapana ndiyo utaratibu wa kura bungeni.Je, hapo demokrasi ipo kweli?Labda wajiunge JF ili kubrush vichwa wao vielimike wapate kuondoka na uchumia tumbo tu.
 
Back
Top Bottom