Waziri Nchemba Awaonya Polisi Matumizi ya Nguvu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameitaka Polisi kutotumia nguvu kubwa katika mambo yasiyokuwa na manufaa kwa wananchi ila nguvu hizo zitumike kupambana na biashara ya dawa za kulevya kwa maslahi mapana ya taifa.

Nchemba ameyasema hayo juzi wakati akifunga mafunzo ya awali ya polisi na uhamiaji, katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi, ambapo zaidi ya wanafunzi 3,000 walihitimu mafunzo hayo.

Alisema polisi ikifanya jitihada za kutokomeza biashara na matumizi ya dawa ya kulevya, kila Mtanzania kwa kabila lake, kwa rangi yake na imani yake atalipongeza jeshi hilo kwa kazi ambayo watakuwa wameifanya.

Alisema wananchi hawataweza kulipongeza jeshi hilo kama litatumia nguvu kubwa ya kupambana na masuala yasiyo na tija kwa wananchi, ambapo aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutekeleza kwa vitendo yale yote waliyofundishwa kwa mujibu wa taratibu za jeshi hilo.

Nchemba pia ameliagiza Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za jeshi hilo, askari Polisi wanaokiuka maadili ya utendaji kazi wao, ikiwa ni pamoja na askari wanaobambikia watu kesi, kupokea rushwa pamoja na kukamata raia kwa kutumia nguvu zisizostahili.

Alilaani pia tabia ya wananchi kujichukuliwa sheria mkononi kama vile kuua watu wasiokuwa na hatia kwa visingizio za imani za kishirikina, pamoja na sheria kutofuatwa kwa watuhumiwa.

Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania- Moshi, Matanga Mbushi, alisema wanafunzi hao wamepewa mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kuongeza kuwa kati ya wanafuzi wanaohitimu, wanafunzi 99 wametimuliwa kutokana na makosa ya nidhamu na mimba
 
Attachments

  • 1.jpeg
    1.jpeg
    40.8 KB · Views: 39
Mbona hakumpa boss wake haya mawazo kabla hajahutubu juzi? Mnatutaka raia kutoa ushirikiano kwa polisi lakini hamuwabani hao mapolisi kujenga mahusiano rafiki ya kujali haki za binadamu kwetu sisi raia!
 
Asimamie utekelezaji wa aliyoagiza.
I.e polisi hawapaswi kuzuia mikutano ya siasa maana ni zao la katiba.
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameitaka Polisi kutotumia nguvu kubwa katika mambo yasiyokuwa na manufaa kwa wananchi ila nguvu hizo zitumike kupambana na biashara ya dawa za kulevya kwa maslahi mapana ya taifa.

Nchemba ameyasema hayo juzi wakati akifunga mafunzo ya awali ya polisi na uhamiaji, katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi, ambapo zaidi ya wanafunzi 3,000 walihitimu mafunzo hayo.

Alisema polisi ikifanya jitihada za kutokomeza biashara na matumizi ya dawa ya kulevya, kila Mtanzania kwa kabila lake, kwa rangi yake na imani yake atalipongeza jeshi hilo kwa kazi ambayo watakuwa wameifanya.

Alisema wananchi hawataweza kulipongeza jeshi hilo kama litatumia nguvu kubwa ya kupambana na masuala yasiyo na tija kwa wananchi, ambapo aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutekeleza kwa vitendo yale yote waliyofundishwa kwa mujibu wa taratibu za jeshi hilo.

Nchemba pia ameliagiza Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za jeshi hilo, askari Polisi wanaokiuka maadili ya utendaji kazi wao, ikiwa ni pamoja na askari wanaobambikia watu kesi, kupokea rushwa pamoja na kukamata raia kwa kutumia nguvu zisizostahili.

Alilaani pia tabia ya wananchi kujichukuliwa sheria mkononi kama vile kuua watu wasiokuwa na hatia kwa visingizio za imani za kishirikina, pamoja na sheria kutofuatwa kwa watuhumiwa.

Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania- Moshi, Matanga Mbushi, alisema wanafunzi hao wamepewa mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kuongeza kuwa kati ya wanafuzi wanaohitimu, wanafunzi 99 wametimuliwa kutokana na makosa ya nidhamu na mimba
Mh. Waziri tuna imani na wewe. Hasa kesi za madawa ya kulevya polisi wanacheza mchezo wa kujenga mazingira ya rushwa kutoka kwa watuhumiwa. Mfano mwaka 2014 mwezi March 2014, Jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vilikamata meli ya Wapakistani na wa Iran ikiwa na shehena ya madawa ya kulevya takribani kilo 800, red-handed lakini cha kusikitisha Kesi hii inapigwa dana dana tu na polisi wa kitengo cha majini (Marine police). Kwa kisingizio cha kufanya uchunguzi. Uchunguzi gani huo unafanywa wakati mtu kakamatwa na kidhibiti? Mheshimiwa Nchemba tunagemea ubadili utendaji kazi wa jeshi la polisi. Hebu angalia kitu
IMG_0194.JPG IMG_0188.JPG
 
Hongera Mh. Waziri una hekima, sifa ambayo kiongozi yeyote anatakiwa kuwa nayo. Tuliiona hekima yako hata wakati ukitafuta kuteuliwa kuwa mgombea U-Raisi kwenye chama chako.
 
Back
Top Bottom