Waziri Nape siku 7 ulizotoa zimepita, waandishi waliokufa kwenye ajali Simiyu hawajalipwa

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Kulitokea ajali mwanza ya waandishi wa habari na watu wengine, ajali ilibeba simanzi na huzuni nchi nzima.

Waziri mwenye dhamana Nape nae hakua nyuma kushiriki bega kwa bega kuiwakilisha serikali.

Lakini akiwa huko tarehe 12 mwezi huu alitoa siku 7 wale waliokufa ajalini wawe wamelipwa chote wanachodai na kutishia kuwa leseni za hizo media anazo yeye hivyo anawapa siku 7.

Kama kawaida wapo waliopongeza na wapo waliokosoa kuwa kwa utaratibu wa kimahakama na namna ya kupata warithi ni ngumu kukamilika ndani ya siku 7.

Hivyo agizo la waziri Nape lilikua haliko sawa pengine hakujua sheria inavyotaka jinsi ya kuwapata warithi.

Sasa ni siku 14 na bado taratibu hata za kupata warithi hazijakamilika achilia mbali hayo malipo aliyotaka walipwe.

Je, Waziri anasemaje? Alikurupuka au kawaongezea muda.
 
Kulitokea ajali mwanza ya waandishi wa habari na watu wengine, ajali ilibeba simanzi na huzuni nchi nzima.

Waziri mwenye dhamana Nape nae hakua nyuma kushiriki bega kwa bega kuiwakilisha serikali...
naye kiazi tu alijaribu kama atasifiwa
 
Ukiwaamini wanasiasa unakuwa umefanya Very Big Mistake..

Wao ni porojo tu,,Lolote ambalo atahisi litamuongezea nguvu kisiasa yeye atapita nalo.
 
Kulitokea ajali mwanza ya waandishi wa habari na watu wengine, ajali ilibeba simanzi na huzuni nchi nzima.

Waziri mwenye dhamana Nape nae hakua nyuma kushiriki bega kwa bega kuiwakilisha serikali...
Yaani hii nchi sio tu hao mawaziri hawajui chochote wanacho kisema, bali Rais mwenyewe inaelekea na yeye haijui katiba inasema nini.
Angalia mambo ambayo amekuwa aikiyafanya kuhusiana na machifu wa Tanzania. Ni kinyume kabisa na katiba. Japo kuwa Comrade Lissu si mpendi kwa matendo yake ya kisalaiti ni uongo ambao amekuwa akiutoa juu ya kujeruhiwa kwake, lakini katika hili niko naye sambamba.

Hapa mwangalie mtu anaye jiita mama na Rais wa nchi anavyo umbuka!

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…