Good People
JF-Expert Member
- Aug 6, 2016
- 945
- 1,819
Mwigulu: 'Lazima tutoe fursa kwanza vyombo vilivyo chini yangu vifanye kazi kabla ya mimi kuzungumza'
Mwigulu:'Wanasema mbona sisemi juu ya kinachoendelea, hii ni Wizara ambayo siyo kila kitu ni habari, Wizara ina vyombo.
=====
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amepiga marufuku Polisi kuwasafirisha wabunge kutoka nje ya Dodoma wanapowahitaji kwa mahojiano.
======
Tumeshtushwa na ukimya wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kushindwa kutoa kauli kwa mambo anayosimamia.
Nchemba anasimamia wizara yenye dhamana ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa kupambana na wahalifu; wezi, magaidi na wote wanaohujumu masilahi ya Taifa na raia wake.
Pia, ni mdomo wa Serikali katika masuala yote yanayohusu amani, utulivu, na usalama. Ukimya wake umechochea watu kuamini madai ya kuwapo kikundi cha uhalifu kinacholindwa na viongozi.
Kuna matukio kadhaa yametokea hivi karibuni, lakini Nchemba amekaa kimya. Machi 17, kituo cha televisheni cha Clouds Media kilivamiwa na watu wenye silaha, tukio ambalo uongozi wa Clouds ulisema aliyeongoza ni kiongozi wa serikali. Pamoja na habari hizo kutangazwa, wamiliki wa kituo kutoa taarifa Jeshi la Polisi, Mwigulu hakuthubutu kuelezea chochote wala kuagiza ufanyike uchunguzi, alikaa kimya.
Hata Jeshi la Polisi, ambalo kwa kawaida likisikia uhalifu unafanyika mahali fulani hukimbilia haraka kudhibiti na kufanya ufuatiliaji, katika suala la Clouds liko kimya. Hadi leo Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro naye yuko kimya. Mazingira au ukimya huo, umesababisha watu kutengeneza picha mbaya dhidi ya Serikali na jeshi hilo kwa ujumla maana aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alifutwa kazi siku aliyopanga kuwasilisha ripoti ya uchunguzi wa kuvamiwa kituo hicho kwa wakubwa zake. Halafu saa chache baada ya kufutwa kazi likafuata tukio jingine baya la yeye kutishiwa kwa bastola na mtu anayeelekea kuwa anafahamika tena mbele ya waandishi wa habari aliotaka kuzungumza nao.
Katika hili Mwigulu alitoa amri mtu huyo afuatiliwe na kuchukuliwa hatua lakini aliishia kusema baadaye kwamba “mtu huyo amejulikana ila si polisi” na ameliacha suala hilo kwa mamlaka husika.
Hadi leo mtu huyo hajakamatwa licha ya sura yake kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari na mitandaoni. Kutokamatwa kwa mtu huyo na kuvamiwa Clouds kumejenga taswira kwamba kumbe kuna watu wanatumwa kufanya uhalifu ndiyo maana hawachukuliwi hatua.
Kabla matukio hayo hayajapoa tulishuhudia msanii Ney wa Mitego akikamatwa na polisi kwa madai ya kutunga wimbo uliokuwa na maneno yaliyodhaniwa ya uchochezi lakini mara aliachiwa kwa amri ya Rais. Ghafla jinamizi la utekaji likamkumba msanii mwingine Roma Mkatoliki.
Kwa kuwa Mwigulu hakuonekana kuwa na msaada, wasanii wenzake walikwenda kwa mkuu wa mkoa kuomba asaidie msanii huyo apatikane naye akawaahidi kuwa angepatikana kabla ya Jumapili iliyopita. Katika hali ya kushangaza Roma alipatikana Jumamosi katika mazingira tata maana wakati Polisi Oysterbay wakitangaza kuwa amepatikana, Kamanda Sirro alikuwa na waandishi akisema hajapatikana. Mbunge wa Jimbo la Nzega, Hussein Bashe alishadadia hoja ya utekaji alipoeleza bungeni juzi kwamba amepata habari kwamba yeye ni miongoni mwa watu 11 wanaotarajiwa kutekwa wakati wowote.
Bashe hakumung’unya maneno alisema habari hizo mbaya dhidi yao alipewa na baadhi ya mawaziri. Matukio haya, kwa vyovyote, yangemfanya Mwigulu atoe msimamo wa Serikali lakini yuko kimya kama waziri asiye na wizara. Tunamshauri Mwigulu kama mambo yanayofanyika ni mazito hawezi kuyafuatilia wala kukemea kwa namna yalivyosukwa, ajitathmini na kuamua ili asiwe sehemu ya uovu huu.
Chanzo: Mwananchi