Waziri Mkuu; utarudi TRA na TPA usipofanya haya

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,981
45,902
Ziara za mara kwa mara za Mh. Waziri Mkuu TPA na TRA, zinamaanisha somo halijaeleweka.

Tatizo ni moja tena kubwa sana. Pale kuna mabwana wakubwa ambao wamekua wakihudumu kwa zaidi ya miaka 20, kiasi kwamba idara zimegeuka korido za nyumba zao, akigeuka anakutana na mkwe, bintie, mjomba, rafiki yake, mtoto wa jirani na kadhalika, kwa kifupi idara za serikali zimebinafishwa.

Ni vigumu sana kufanya mabadiliko kwa hali hiyo tajwa hapo juu, watu wanafahamiana kwa undani na wanalindana, uozo ndio umetamalaki.

Cha kufanya, hizi taasisi mbili zivunjwe, ajira zitangazwe upya waajiriwe wafanyakazi wengine kabisa ambao hawataendeleza uozo. Kuna watanzania wengi tu ambao ni wazalendo na qualified, hakuna haja ya kung'angania watu, what is the use ya kuwasomesha kama hatuwaamini kwa kuwapa majukumu ya kulitumikia taifa lao.

Sio vibaya ku start all over, au bila hivyo safari za TRA na TPA zitakua after every one month.

Ukiachana na hilo kuna jingine la uhujumi uchumi ambalo ni pana, kuna adui wa nchi ambao wanaweza tumia mianya ya kupenda rushwa kwa watumishi wa uma kuwarubuni ili kuhujumu mapato ya nchi.

Katika kuajiri watu upya, vyombo vya dola vyote vishiriki katika zoezi la uajiri kwa vetting za kutosha kwa kila atakayeajiriwa ili kupunguza mianya wa kuwaajiri mamluki na wahujumu wa taifa hili.
 
Uko sahihi,subiri tuwaone wahusika kwa majibu ya ushauri huu.
 
Kwa Tanzania yetu hii sahau. Watanzania sisi ni wanafiq na kujifanya wakarimu.

Only honesty and hardworking is needed. Ukiona madudu wanaojiita wasomi wanayoyafanya inakukatisha tamaa hata wenye elim ndogo kama yangu kusita kurudi shulen na kujiendeleza.

Ubinafsi ulioko miongoni miongon mwetu inatufanya tusiwe wazalendo.
 
Ushauri mzuri sana.Haiwezekani serikali kuu kuhamia TPA na TRA na hatuoni tofauti kila siku yanazuka mapya.JPM na MKM ni ushauri wa bure acheni udikiteta
 
Ushauri mzuri sana.Haiwezekani serikali kuu kuhamia TPA na TRA na hatuoni tofauti kila siku yanazuka mapya.JPM na MKM ni ushauri wa bure acheni udikiteta
Hakuna sababu ya kuzivunja. Wawafanyie transfer kwenda kwinginr serikalini. Mhasibu Wa Tra,TPA anaweza kuwa mhasibu Halmashauri, tamisemi, Wizarani nk. Japo wanaita sehemu hizo makaburini (hamna hela)
Kuacha watumishi eneo moja muda mrefu ofisi zimegeuka Mali yao.
 
Back
Top Bottom