Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, naye ajitosa bunge live

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,911
2,891
Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu aliyehudumu katika nafasi hiyo tangu mwaka 1995 hadi 2005 mheshimiwa Fredrick Sumaye amesema suala la kuzuia kurusha matangazo ya bunge live ni uvunjifu wa Katiba na ukiukwaji wa haki ya watanzania kupata habari.

Amesema hayo leo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Habari.

Najaribu kujiuliza hivi ni nani aliishauri serikali kutekeleza ubabe huu?

===============

FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu ameeleza kushangazwa na Serikali ya Rais John Magufuli kupenda kusifiwa zaidi na kuchukia kukosolewa,
maxresdefault-620x308.jpg

Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu

Sumaye bila kumtaja jina Rais Magufuli ameleza kushangazwa na hatua ya serikali kuminya uhuru wa habari na kwamba, kufanya hivyo kunalenga kuficha madudu yanayofanywa na watendaji wake.“Wapowatawala ambao hawapendi kusemwa lakini wanapenda sana kusifiwa.

Kiongozi mwenye tabia ya udikteta hataki kusikia kingine zaidi ya sifa zake tu. “Huyo ni mtu hatari na katika nchi ya namna hiyo hakuna uhuru wa habari wala uhuru wa kutoa maoni kwa woga wa kupotezwa kusikojulikana,” amesema Sumaye.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habri za Siasa (TAPOREA), Sumaye amesema, serikali inakiuka Katiba ya nchi. Amesema, serikali yoyote inayopambana na vyombo vya habari na kuminya uhuru wa kufanya kazi zao huwa ina tatizo kwa upande wa wanaotawala.

Akitolea mfano wa hatua ya serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya bunge Sumaye amesema, kwa kufanya hivyo serikali imevunja Katiba.“Unapoondoa matangazo ya moja kwa moja ya vipindi vya Bunge, kwanza ni kuvunja katiba. Ibara ya 18 (d) ya Katiba inasema, kila mtu ana haki ya kupewa taarifa wakati wote.

“Kwa kuzuia Bunge kuoneshwa ‘live’ (moja kwa moja) wewe serikali unataka kutoa taarifa ya Bunge kwa wakati unaoutaka na kwa taarifa unayoitaka wewe,” ameeleza Sumaye. Kuhusu sababu iliyotolewa kwamba, matangazo hayo yanatumia gharama ya Sh. 4 bilioni amesema haina mashiko.

Sumaye amesema, hata kama matangazo hayo yatarushwa na ofisi za bunge bado, gharama zitaongezeka zaidi kwa sababu Bunge litahitaji kununua mitambo pamoja na kuajiri wafanyakazi wake.

Sumaye amesema, serikali yenye demokrasia ya kweli lazima ikubali wananchi wake kutoa maoni. “Serikali yoyote yenye utawala bora, ingependa mambo yake inayoyafanya kwa ajili ya wananchi wake mambo hayo yajulikane kwa wananchi hao. “Ukiona serikali inaficha mambo yake lazima kuna mambo wanayoyafanya ambayo hayafai na wasingependa jamii ijue,” amesema Sumaye.

George Maziku, Mkurugenzi Mtendaji wa TAPOREA amesema, ripoti ya hali ya uhuru wa waandishi wa habari na uhuru wa vyombo vya habari kimataifa, iliyotolewa na Shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka lenye Makao Makuu yake nchini Ufaransa haipendezi.

Amesema, ripoti hiyo inaonesha kuwa, katika miaka 10 iliyopita zaidi ya waandishi wa habari 800 kutoka mataifa mabalimbali duniani wameuawa wakiwa wanatekeleza kazi zao.

“Kitisho kingine kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini ni utamaduni mpya ulioasisiwa na kuimarishwa na watawala wa sasa na kuvishinikiza vyombo vya habri kutomkosoa Rais John Magufuli na serikali yake. “Matokeo yake, vyombo vingi vya habari nchini vimelazimika kuandika habari za kumfurahisha Rais Magufuli,” amesema Maziku.
 
Kwa sasa wanajitoa kuwa serikal haihusiki, na wanadai waliokata matangazo ni bunge wao kisa bunge limeanzisha studio yake yakurusha matangazo, ngoja wajifungie na waamue wenyewe ss wananchi hatujui kinachozungumzwa wala kinachoendelea.....sabab eti tunaisoma namba
 
  • Thanks
Reactions: 999
waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu aliye hudumu ktk nafasi hiyo tangu mwaka 1995 hadi 2005 mheshmiwa fredrick sumaye amesema suala la kuzuia kurusha matangazo ya bunge live ni uvunjifu wa katiba na ukiukwaji wa haki ya watanzania kupata habari. amesema hayo leo ktk kilele cha maadhimisho ya siku ya habari. najaribu kujiuliza hivi ni nani aliishauri serikali kutekeleza ubabe huu?
Hilo swali waulize CLOUDS FM, maana ndiyo washauri wa CCM siku hizi.!
 
Hii kitu sijawahi ona hata nch za jilan watatuina sie baboguz kias mpaka tuna fugia wananch kuona kinachojadiliwa,kweli watu tungekuwa na hakili moja na fikila za kuelewana ccm wangetukoma.
 
penye ukweli usifiche hisia zako suala la bunge kutorushwa live limepunguza furaha ya watanzania wengi na wengi wao kubaki wananung,unika
 
Swala hili la kuonyesha bunge live kama halina baraka za magufuri basi ni mkakati wa makusudi hili serikali ya magufuri uchukiwe kumbuka magufuri hotuba zake nyingi anawaomba wananchi wamuombee haiwezekani magufuri huyo huyo aunge mkono wananchi wake wasione wawakilishi wao bungeni tafakari!
 
amesema suala la kuzuia kurusha matangazo ya bunge live ni uvunjifu wa katiba na ukiukwaji wa haki ya watanzania kupata habari.

Muulizeni kipengele gani katiba kimevunjwa!!!!!
Ofisi zote zikiwemo za taasisi,serikali na vyama vikiwemo CUF,CHADEMA na NCCR zina maofisa habari ambao kazi zao zao ni kutoa habari zao.Bunge lina maofisa habari pia kaenda kuzitafuta hizo habari akanyimwa? Aende studio ya bunge wakampe hizo habari anazotaka yeye au mtanzania yeyote.

Kikao cha bunge ni kikao cha kikazi sio mkutano na waandishi wa habari (press conference).kuna tofauti ya kikao cha kikazi na press conference! Wanaotaka kugeuza bunge kuwa press conference ambamo muda wote waandishi wa habari wamo hawako sahihi

Wabunge wakishakaa na kumaliza kazi ya siku ndio taarifa za yale muhimu ya kazi na matokeo waliyofikia yanawekwa hadharani na maofisa habari wa bunge

Taarifa hizo haziwi na vitu vya kipuuzi kama vile vya mbunge gani amemtukana waziri au mbunge fulani kwa kumwita Kibaka nk.Zinakuwa na zile taarifa muhimu tu za kazi waliyofanya kwenye vikao.

Ikumbukwe pia kuwa Vikao vya kamati za bunge huwa havirushwi Live sababu ni vikao vya kikazi.Na kikao cha bunge ni kikao kikuu cha kikazi sio press conference .Sasa hivi wabunge watafanya kazi barabara kuliko zamani ambapo mara ingine mtu anaomba kuchangia ili tu auze sura kwenye TV aonekane.Wachangiaji unakuta wako msururu wakipigania tu kuonekana!!! Sasa hivi bunge litakuwa na wachangiaji very serious ambao wana hoja za nguvu na si wauza sura kwenye TV

Bunge la Tanzania litakuwa bunge la mfano la kuigwa duniani kwani litatoka na vitu serious vilivyofanyiwa kazi barabara na wabunge serious na habari zitakazotolewa ni zile za HAPA KAZI TU na si zile za mara mbunge kapigwa picha anasinzia bungeni nk

Pia Kazi kuu ya mbunge (Major duty) ni kuleta maendeleo kwenye jimbo lake anakotokea na si kuongea sana na kuchonga sana mdomo bungeni na kuanika sura sana kwenye kamera za Televisheni akiwa bungeni.Kuna wabunge majimboni hata kuwaona na kuwakuta ofisini kwao majimboni ni shida.Wao husubiri tu muda ufike wa bunge wachonge midomo na kuuza sura kwenye TV.
 
Waziri husika ndio chanzo.nchi hii hakuna usawa kabisa.wananchi hatupati haki yetu ya habari.kwa kweli inauma sana.
 
Swala la TBC kutumia billion 6 kwa mwaka kwa ajili ya kurusha bunge live wakati watanzania 70% wako vijijini hawana TV wala umeme ni upuuzi mtupu...
 
Muulizeni kipengele gani katiba kimevunjwa!!!!!
Ofisi zote zikiwemo za taasisi,serikali na vyama vikiwemo CUF,CHADEMA na NCCR zina maofisa habari ambao kazi zao zao ni kutoa habari zao.Bunge lina maofisa habari pia kaenda kuzitafuta hizo habari akanyimwa? Aende studio ya bunge wakampe hizo habari anazotaka yeye au mtanzania yeyote.

Kikao cha bunge ni kikao cha kikazi sio mkutano na waandishi wa habari (press conference).kuna tofauti ya kikao cha kikazi na press conference! Wanaotaka kugeuza bunge kuwa press conference ambamo muda wote waandishi wa habari wamo hawako sahihi

Wabunge wakishakaa na kumaliza kazi ya siku ndio taarifa za yale muhimu ya kazi na matokeo waliyofikia yanawekwa hadharani na maofisa habari wa bunge

Taarifa hizo haziwi na vitu vya kipuuzi kama vile vya mbunge gani amemtukana waziri au mbunge fulani kwa kumwita Kibaka nk.Zinakuwa na zile taarifa muhimu tu za kazi waliyofanya kwenye vikao.

Ikumbukwe pia kuwa Vikao vya kamati za bunge huwa havirushwi Live sababu ni vikao vya kikazi.Na kikao cha bunge ni kikao kikuu cha kikazi sio press conference .Sasa hivi wabunge watafanya kazi barabara kuliko zamani ambapo mara ingine mtu anaomba kuchangia ili tu auze sura kwenye TV aonekane.Wachangiaji unakuta wako msururu wakipigania tu kuonekana!!! Sasa hivi bunge litakuwa na wachangiaji very serious ambao wana hoja za nguvu na si wauza sura kwenye TV

Bunge la Tanzania litakuwa bunge la mfano la kuigwa duniani kwani litatoka na vitu serious vilivyofanyiwa kazi barabara na wabunge serious na habari zitakazotolewa ni zile za HAPA KAZI TU na si zile za mara mbunge kapigwa picha anasinzia bungeni nk

Pia Kazi kuu ya mbunge (Major duty) ni kuleta maendeleo kwenye jimbo lake anakotokea na si kuongea sana na kuchonga sana mdomo bungeni na kuanika sura sana kwenye kamera za Televisheni akiwa bungeni.Kuna wabunge majimboni hata kuwaona na kuwakuta ofisini kwao majimboni ni shida.Wao husubiri tu muda ufike wa bunge wachonge midomo na kuuza sura kwenye TV.
nashangaa, mbona hufanani na unayoyasema na jinsi ulivyo tofauti, nilifikiri una uwezo wa kuchambua mambo kumbe siyo
 
Back
Top Bottom