bomouwa
JF-Expert Member
- Jun 19, 2014
- 1,149
- 798
Habari wanajamvi,
Kwa walioangalia habari za ITV saa mbili hii. Kuna habari ya Mh.Waziri mkuu kutoa agizo/Amri yani sijui nisemeje,juu ya kauli yake ya kuagiza (hapa naomba kunukuu "HALMASHAURI AMBAZO HAZITAKUSANYA MAPATO KUANZIA 80% BASI ATAZIFUTA").
=================
UPDATE
=================
Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Halmashauri yeyote itakayoshindwa kukusanya mapato juu ya asilimia 80 kuanzia hivi sasa serikali itaifuta huku akiendelea kutahadharisha kuwa vita dhidi ya rushwa na ufisadi ni ya kudumu ndani ya serikali ya awamu ya tano.
Mh. Waziri Mkuu Kasim Majaliwa ameyasema hayo katika wa mkutano mkuu wa jumuiya ya tawala za mitaa Tanzania ALAT ambapo amesema moja ya changamoto inayoikosesha serikali mapato ni rushwa na kuwataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele kuchukia rushwa na ufisadi unaoligharimu Taifa na kuhakikisha mapato ya kwenye kila halmashauri yanaongezeka kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji kodi na ushuru wa kielektronoki.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo anasema kuwa endapo viongozi wa halmashauri watasimamia vyema maeneo yao kuna kila sababu ya Tanzania kusonga mbele katika nyanja ya maendeleo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa ALAT Taifa Gullam Hafidh Muqaddam amesema ameitaka serikali kupeleka ruzuku katika halmashauri kama inavyoainishwa kwenye bajeti ili kuharakisha maendeleo na kuondoa misuguano baina ya watendaji wa halmashauri na wananchi.
Chanzo: ITV
Mawazo yangu
Kwa mujibu wa "experience" inaonyesha maneno mengi ya viongozi huwa yanaongelewa pasi kua na tafiti za kisayansi kujua umuhimu ama athari za jambo fulani. Sasa nilichojaribu kujiuliza ni kama ifuatavyo:
1.Nini kipimo kilichotumika kujua ukusanyaji wa kodi wa 80% kwa kila halmashauri?
2.Kuna tofauti kubwa za kiuchumi zilizomo kati ya halmashauri na Halmashauri mathalani ukusanyaji wa halmashauri ya K'ndoni ni tofauti na Rufiji(huu ni mfano), je,unaposema 80%hapa kuna usawa wa ukusanyaji?
3.Kwanini Mh. Waziri mkuu amesema 80% na sio 60%? Nitashukuru kwa masahihisho kwa wale walitazama habari hii.
Nawasilisha.