Waziri Mkuu asema Tanzania kuanza kuiuzia umeme Zambia

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,880
6,366
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania ina mpango wa kujenga njia ya umeme kutoka Mbeya hadi Zambia kupitia Tunduma ili kupunguza tatizo la umeme linaloikabili nchi hiyo.

“Serikali ya Tanzania inajenga njia ya umeme ya msongo wa KV 400 kutoka Iringa - Dodoma – Singida – Shinyanga ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa umeme unaolenga kuunganisha Zambia, Tanzania na Kenya,” amesema.

Amesema upembuzi yakinifu kwa ajili KV400 kutoka Iringa hadi Mbeya umekwishakamilika tangu mwaka 2012, na hivi sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili kuunganisha kipande cha kutoka Mbeya na gridi ya Taifa ya Zambia.

Waziri Mkuu ambaye anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, ametoa ufafanuzi huo leo mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa wakuu wa nchi na Serikali uliohusuNishati na Mabadiliko ya TabiaNchi kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi.

Amesema ili kukabiliana na changamoto ya nishati barani Afrika, nchi za bara hili zinahitaji kuwa na fedha ama mitaji, teknolojia ya kisasa na wataalamu wenye ujuzi wa kutosha jambo ambalo amesema ni gumu kulikamilisha kila nchi peke yake.

Amesema ili kukaribisha wawekezaji kwenye sekta ya umeme, Tanzania inafanyia marekebisho sheria zake ili kuruhusu uwekezaji kwenye sekta hiyo.

Akizungumzia kuhusu hali ya nishati Tanzania, Waziri Mkuu alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na gesi asilia yenye ujazo wa futi trilioni 57.25 (tcf), makaa ya mawe yenye uhjazo wa tani bilioni 1.9 (asilimia 25 imevumbuliwa), umeme wa nguvu ya maji wa gigawati 4.7 ambazo ni asilimia 12 tu ndiyo inatumika. Pia alisema Tanzania ina deposits za urani yenye ujazo wa ratili milioni 200 (200 million pounds), joto la ardhini (geothermal) linaloweza kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 5,000. “Hivyo ni mbali na vyanzo vya umeme utokanao ua upepo na jua,” alisema.

Akizungumzia kuhusu usambazaji wa umeme vijijini, Waziri Mkuu alisema Tanzania kupitia REA imefanikiwa kusambaza umeme kwenye asilimia 52 ya vijiji vyote na inatarajia kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2025.

Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.

“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,” alisema.

Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário

Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.

“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,” alisema.

Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema masuala ya nishati yanahitaji uwekezaji mkubwa kwa hiyo akashauri makampuni kuungana kwenye uwekezaji na kuibua miradi ambayo ina tija (feasible and viable).

Waziri Mkuu amefuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu Kijaji, wachumi kadhaa pamoja na wataalamu wa sekta ya fedha.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MEI 24, 2016.
 
Hii poa sana. Tanzania sasa inapiga hatua kubwa sana. Tunategemea mda mfupi sana tutaanza kufurahia matunda ya Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli. MMKM.
 
Jana tumelala usiku kucha bila kuwa na umeme halafu jamaa wanaongelea kuuza umeme Zambia. Hivi kwanini wasijikite kwenye kumaliza taizo la umeme nchini kwanza kabla ya kuwaza kuuza nje ya nchi umeme ambao hautoshelezi mahitaji ya ndani?
 
sawa na kumpelekea jirani yako mke wako baada ya yeye kufiwa na Mkewe ili update sifa
 
Jana tumelala usiku kucha bila kuwa na umeme halafu jamaa wanaongelea kuuza umeme Zambia. Hivi kwanini wasijikite kwenye kumaliza taizo la umeme nchini kwanza kabla ya kuwaza kuuza nje ya nchi umeme ambao hautoshelezi mahitaji ya ndani?
Mi huwa nashangaa mnamlaumu nape haaa sijui vuvuzela hata huyu kiongozi wao ni vuvuzela mkuu ivi umeme huu wa kuunga unga ndo watauza au umeme kwa maana ya ukimwi?aaahh mi sijaelewa mabwawa yenyewe haya na miundombinu ya ovyo hii. Waanza kuuza sukari kwanza umeme baadae
 
Jana tumelala usiku kucha bila kuwa na umeme halafu jamaa wanaongelea kuuza umeme Zambia. Hivi kwanini wasijikite kwenye kumaliza taizo la umeme nchini kwanza kabla ya kuwaza kuuza nje ya nchi umeme ambao hautoshelezi mahitaji ya ndani?
Subiri grid kubwa inajengwa. Ikimalizika utakuwa happy.
 
Kuna muda India na Kenya ndo walikuwa wanaongoza kwa kuuza Tanzanite ;madini yanayopatikana Tanzania pekee.
 
Serikali ya wakurupukaji haiachi maigizo. Miezi michache iliyopita, waziri Muhongo aliwaambia watanzania kwamba serikali inatarajia kununua umeme wa bei nafuu toka Ethiopia leo wanasema wataiuzia umeme Zambia wakati ilipogunduliwa gesi kule Mtwara tuliaminishwa kwamba Tanzania itauzia umeme nchi nyingi za jirani. Hivi hawa jamaa mbona hawaeleweki eleweki?
 
Jana tumelala usiku kucha bila kuwa na umeme halafu jamaa wanaongelea kuuza umeme Zambia. Hivi kwanini wasijikite kwenye kumaliza taizo la umeme nchini kwanza kabla ya kuwaza kuuza nje ya nchi umeme ambao hautoshelezi mahitaji ya ndani?

Mkuu..
Picha na Viongozi ndilo lilikua la Muhimu..
Huo Umeme Watausubiria hadi Yesu atakapo rejea
 
Hii poa sana. Tanzania sasa inapiga hatua kubwa sana. Tunategemea mda mfupi sana tutaanza kufurahia matunda ya Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli. MMKM.
Inapiga hatua kwa matamko? Mpaka sasa ili kutosheleza mahitaji yenu ya ndani mnahitaji MW ngapi?
mtakuwa mataahira mpaka lini?
 
Huu ni ukichaa wa standard gauge.
Ila kwasababu rais ameteua mshauri wa mambo ya kiuchumi jana labda huu ujuha utaenda unapungua.
 
Shida kubwa ya viongozi wengi wa Afrika hawana Vision... Hawana vipaumbele achilia mbali mipango ya muda mrefu na ya kati!! Wao kila kitu wanataka paramia ili waonekane!! Mwisho wa siku wanajikuta hawajafanya lolote! Nchi haina umeme wa kutosha na wa uhakika!! Nchi haina nishati ya umeme kuvutia viwanda vikubwa!! Lakini less than 30% ya watanzania hawana umeme then hawa viongozi wanakurupuka kuhangaika kupeleka umeme Zambia!! Nani katuroga??

ujamaa ni laana inayoitafuna nchi hii.
 
Nchi ya wadanganyika na wapiga dili.

Matapeli siku zote wanatapeli kwa kujenga mazingira ya kuaminika kwanza.
Huwezi kumwibia mtu kwa kumtapeli bila kumjengea mazingira ya kukuamini.

Juzi tumeambiawa kuwa Tanzania tunampango wa kununua umeme toka Ethiopia kupitia Kenya.
Sasa leo tunaambiwa tutawauzia Zambia.
Umeme wa ndani wenyewe bado kuusambaza nchi nzima.

Tumeamua kuwekeza au kununua umeme kwa bei nafuu toka Ethiopia.
Sasa tuangalie unafiki serikali ya CCM; wanatuambia kuwa wanalinda viwanda vya ndani lakini wanashindwa kuwekeza kwenye umeme na kuwauzia majirani bila kuingiza umeme tola Ethiopia.
Miradi ya Tz inajengwa kwa gharama kubwa kubwa sana ndio maana hata huduma zake zinakua za ghali sana.
Maporomoko ya stiglers kule Rufiji yanaweza kuzalisha umeme mwingi sana wa bei nafuu kabisa lakini sisi tunakimbilia umeme wa gas unaohitaji vipuri na mindo mbinu ya ghrama kubwa sana
 
Sielewi. Tunaweza kuuza umeme kwa nchi jirani wakati chini ya asilimia 50 ya watanzani hawana umeme? tunalenga nini hasa?
 
Serikali ya wakurupukaji haiachi maigizo. Miezi michache iliyopita, waziri Muhongo aliwaambia watanzania kwamba serikali inatarajia kununua umeme wa bei nafuu toka Ethiopia leo wanasema wataiuzia umeme Zambia wakati ilipogunduliwa gesi kule Mtwara tuliaminishwa kwamba Tanzania itauzia umeme nchi nyingi za jirani. Hivi hawa jamaa mbona hawaeleweki eleweki?

Hahahaha.....Hii ndio Tanzania...Twendeni tu...Tutajua mbelekwa mbele huko
 
Hii poa sana. Tanzania sasa inapiga hatua kubwa sana. Tunategemea mda mfupi sana tutaanza kufurahia matunda ya Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli. MMKM.
Kipi hasa umekiona ni poa? Kuwapelekea Zambia umeme wakati sisi hatujitoshelezi? Kijijini kwetu nimelipia umeme tangu last year mwezi wa nane mpaka leo hata nguzo hatujaziona.
 
Back
Top Bottom