Waziri Mkuu akiwa mapumzikoni Jimboni Ruhangwa

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
KIJIJI.jpg
 
Jamani jamani jamani wamjengee nyumba haraka, hata kama ya mkopo atalipa taratibu mweeeeeee
 
Ni vema sasa viongozi wa juu wanaenda likizo kwa wapiga kura wao. Ila hiyo misaaada anayopewa na wachina inanipa shaka kwa jinsi navowajua wachina. Pia naona tatizo la katiba yetu kuwa na waziri mkuu na mawaziri wenye majimbo, hii inasababisha kuwa na double standard kwenye utekelezaji wa ahadi ukiacha swala la kubana ajira kwani mtu mmoja anakua na ajira mbili kubwa zenye mishahara mikubwa wakati kuna watu hata hizo ajira za mishahara midogo hawapati. Mfano waziri mkuu/waziri wa kawaida kulingana na nafasi yake ni rahisi kupata misaada kutoka kwa mataifa na watu mbalimbali kuliko mbunge ambaye hana uwaziri.

Hili jambo ndo huwa linanifanya naichukia CCM na wabunge wake kila napokumbuka jinsi walivoingiza siasa kwenye bunge la katiba, tena nakumbuka JK alisema "Ndugu zangu wabunge humu kwenye katiba ya Warioba kuna mambo mengi ya kujadili mfano swala la wabunge kutokua mawaziri, tuangalie hili tunakua tunajinyima fursa" Dah kiukweli nilipatwa na ganzi ya masikio, yani jambo la msingi kama hilo mtu anasema ni kujinyima fursa!!!!!!!??????.
 
Bado tunasafari ndefu sana. Cha ajabu unaweza kuta waziri haoni cha ajabu chochote hapo na hyo nyumba ndio yenye afadhali katka kijiji icho
 
Nyumba yake karibia inaisha!!! Sio hiyo!hapo nadhani anasalimia ndugu na jamaa! Wanajenga hata kiwanja kidogo cha ndege!! Kila shirika la huduma limeenda huko! Tanesco maji makampuni simu etc....huduma zote muhimu zipo! Nyumba yake inamaliziwa haraka iwezekanvyo! Ila waliomzunguka ndio hatari sasa kama hivyo! Korosho wanadhulumiwa kodi zimekuw nyingi sana! Mikorosho imechoka sas inatakiwa ipandwe mingine! Pia wadudu wanashambulia , maisha yako Duni sana mikoa ya kusini!
 
Wapi imeandikwa kwamba hapo ndio kwa waziri mkuu? Umekurupuka.

Alafu sioni ubaya wa hiyo nyumba maana ndio asili ya maisha ya huko.
Umekurupuka kujibu kwa lugha ya kukwaza, ungeweza kutumia lugha ya kistaarabu tu na ukaeleweka Leo sijui umekuwaje, umekuwa kama uvccm
 
Sifa za kijinga kujipigisha picha ili uonekane unajali maskini..!

Yeye hapo anapokea milions of money kwa mwezi..!

Kukaa na hao maskini kijiweni na kupiga picha, na kuondoka hakutawatoa kwenye hizo nyumba za matope.

Afanye kazi yake;

Hii serikali ya mapicha picha inanikera. Fanyeni kazi bhana!
 
Back
Top Bottom