Waziri Mambo ya ndani ajaye; Hali ya usalama wa raia ni mbaya, anza na haya

lars

Member
Jan 16, 2015
89
142
Ndugu wanabodi,

Wakati tunashangaa kizazaa cha swala la Lugumi na lile la wanafunzi wa UDOM kurudishwa nyumbani bila makosa yao, kuna mambo makuu 3 ambayo naomba tuikumbushe serikali yetu iweze kuyasimamaimi kikamilifu.

1. Hali ya usalama wa raia na mauwaji wa kutisha.
Katika siku za hivi karibuni, tumesikia na kushuhudia mauwaji ya kutisha katika mikoa kadhaa ya Tanzania..kama vile lile la polisi Trafiki kuuwawa, watu kadhaa msikiti wa Mwanza, dada yake ya biolinnea Msuya na jana mauwaji ya huko Tanga. Boda boda nazo zimekuwa zikeendelea kutumika kufanya uhalifu na mauwaji hata mchana kweupe. Mpaka sasa sijiaona mikakati yoyote wa Naibu Waziri M/ndani na jeshi la polisi inayoweza kutatatua haya maswala.

Nashawishika kusema sasa, sisi wananchi tuseme haya basi, yametosha. Viongozi tuliowachagua wafanye kazi yao na siyo kila swala lisubiri Mhe. Rais JPM aingile kati. Hivi mawaziri,wakuu wa mikoa, wilaya, mitaa, polisi, kamati za ulinzi, mnafanya nini? Mapendekezo yangu

a) Kuna haja sasa ya Polisi na kamati za ulinzi za wilaya na mitaa, kuja na mikakati makini ambayo wataisimamia katika ngazi zote kuanzi mitaa. Sielewi kabisa hili dude” Kamati ya ulinzi za mikoa na wilaya zinafanya nini”? Zimekaa tu kusubiri posho?

b) Kurudushiwa ulinzi wa mitaa na SUNGUSUNGU. Ulinzi wa raia unaanzia kwa raia wenyewe. Tukirudishwa huu ulinzi tunaweza kudhibiti wahalifu wanaofika mitaa yetu, hasa kwa kutumia boda boda. Hatuwezi kukosemsha mauwaji kwenye kaya za watu bila ya kuimarisha ilinzi wa mitaa. Lakini lazima serikali ituongoze kwa kuwa na kusimamia karibu na kuwa na viongozi shupavu (Pamoja na mapugufu ya Mrema kisiasa, natamani Mrema Lyatonga angekuwepo kwa hii wizara)

c) Raia sasa waanze kutemebea na ID zao , hata ambaye hana basi apate barua ya kumtambulisha toka Serikali ya mtaa

d) Huenda mitandao ya Alshabab na ISIS imeshangia, sasa supermarket zote , vyuo , makanisa, Misikiti etc, yawe vifaa vya kugundua siraha na kufanya inspection kwa kila raia au gari inayo ingia pale. Mbona Kenya na Uganda tu hapa wanafanya. Jamani hapa mnashindwa nini? Mpaka tufe? Yaani hawa jamaa kama wataanza , watatumaliza kama kuku, kwani tumejikalia tu bila tahadhari yoyote. Waziri, mkuu wa polisi, mnasubiri mpaka Rais awaambie hili?Viongozi kuweni wabunifu jamani.

2. Udhibiti wa polisi kwa ajali barabarani
Ingawa nawapongeza Jeshi la polisi kwa kushirikiana SUMATRA, kupunguza ajali za barabarani, bado hali yaijawa ya kuridhisha. Najua swala la ajali siyo polisi tu, bali hata sisi Drivers na Raia. Hata hivyo uzembe wa kuendelee kuruhusu magari/mabasi mabovu , Drivers waliolewa , mwendo kasi usiofata ratiba, Trafiki polisi bado wanatakiwa kuisimama kikamilifu. Swala hili la ajali tusipokuwa makini litatumaliza, na lisikieni tu kwa wengine. Siku ambayo ndugu au rariki yako limemepata , ndo mtakapoona uchungu wa kukatisha maisha kunakoweza kuzuilika. Napendekeza yatuatayo.

a) Polisi na SUMATRA msimamie kidete sheria za babarani . Rushwa sasa ithibitiwe kikamilifu kwa kutumia Takukuru-wasafiri

b) Wananchi na Drivers, tutoe ushirikiano wa kufata sheria barabarani

c) RUSHWA na polisi Idhibitiwe. Kwa kweli nadhani mabadilijo makubwa yanahitajika katika kuhakikisha jeshi la polsi linajisafishwa wa walio wachache ambao hujihusisha na rushwa na hivyo kuwaacha watanzania wakifa na ajali. Pia kitendo cha polisi mikoani kuomba hela ya faini bila risiti ya za serikali za yellow, linatia shaka maama hatujui hizo hela zinafika serikalini. Polisi anakwambia kitabu sina au mpaka twende kituo kikuu. Hivi Kamamnda Mpinga umeshindwa nini kugawa hizo machine na pia Vitabu vya risiki vya serikali wa polisi wako na wale wanaosumbua raia kwa kutokuwapa risiti au kuwapiga danadana uwaondoe? Tutengezee Whatsapp ya Jeshi la polis, sis tutakuwa tunakurushieni picha za hawa Polisi wenzako wakorofi.

d) Bodaboda pia wafate sharia kaka magari. Unakuta polisi anamwacha kumkamata boda boda anayepita kwenye red-trafiki light. Mime nimeendesha pikipiki Ulaya, sikuwahi kuona

piiki piki zinarufusuwa kupita kwenye taa nyekudu. Hili lidhibitiwe mapem. Nchi kama Rwanda bodaboda zina nidhamu na sheria zinafuatwa. Hapa polisi mnashindwa nini? Nalo hilo mpaka aje Magu? Kamanda Mpinga umelala hata boda boda tu wanakushinda?

3. Foleni
Pamoja kuwepo tatizo la miundombinu, foleni, kwa kiasi kikubwa inachangiwa na raia wenyewe hasa kwa kuchomekea magari ya Raia, serikali na daladala. Ifike muda sasa (suhuhisho la muda mfupi)

a) Polisi wakamate magari yote ya serkali yanayochepuka. Kama wakubwa wetu wana haraka, basi wawe wana amuka mapema au kuanza safari mapema

b) Daladala, ni shida. Kuna haja sasa ya kutumia kamera kama 200 za zoom kwa Dar, amabazo ziataweza kureko matukio ya magari umbali hata wa km 1. Drviers wakorofi wanaochepuka kuweza kukamatwa mbele ya safari . Hii siyo gharama kubwa kama nchi imedhamiria. Hata mimi naweza kukunua hizi Kamera kwa mshahara wangu halali. Hakuna haja ya kuwafanya Trafiki wawe kila mahali , Tuwape nyenzo na pia nao waache Rushwa.

c) Kama nilivyosema hapo juu, Jeshi polidi na mawaziri husika muwe wabunifu wa kutatua matatizo mapema. Fungueni WhatsAPP account na sisi raai wema tuwekuwa tunarekosi Drivers wahalifu na wanaochepukaji na kuwarushia nyinyi direct na kuwakamata.

Mhe. Rais, tunaomba utuletete Waziri M/Ndani ambaye atakuwa shupavu kweli kweli kusimamimia uhalifu, rushwa , kukarabati upya jeshi la polisi. Natumaini utatuletee mtu ambaye ana uchungu na hii nchi na siyo kutuletea watu ambao waliokaa hiyo wizara wakaruhusu mitandao wa ujambazi iliopo sasa ikatanda(najua file zao unazo).

Nawakilisha
 
Back
Top Bottom