Waziri Majaliwa: Serikali imelipa jumla ya sh29 bilioni kwa watumishi wa umma

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,850
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imelipa jumla ya Sh29 bilioni kwa watumishi mbalimbali wa umma wakiwemo walimu ikiwa ni sehemu ya madeni yao.

Majaliwa amesema hayo wakati wa uzinduzi wa vyumba vitatu vya kisasa vya madarasa katika shule ya sekondari Iwawa iliyoko wilayani Makete.

Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kumaliza madeni ya watumishi hao, ambapo hadi kufikia Novemba mwaka jana kiasi hicho cha fedha kililipwa kwa watumishi 31,000.

Chanzo:Mwananchi
 
Back
Top Bottom