Waziri Magufuli na Barabara ya Bwanga - Biharamulo

Waziri Magufuli na Barabara ya Bwanga - Biharamulo

kanaku

Member
Joined
May 13, 2013
Posts
9
Reaction score
5
Napenda kutumia nafasi hii kutoa dukuduku langu. ni miaka kadhaa sasa tangu mheshiwa Magufuri kuitenga kwa makusudi wilaya ya Biharamulo kwa kuinyang'anya barabara ya rami na hatimaye kuiacha katika lindi kubwa la umasikini kwani hata barabara iliyopo kwa sasa ni aibu tupu. ukisafiri kwa gari ikitokea mkoa wa Geita mwisho wa uhai huishia "Bwanga" ambapo barabara ya rami huchepuka kuelekea Chato na hatimaye Bukoba na kuiacha ile ya Biharamulo katika hali tete, kwani ukiingia kule utadhani umeingia Dunia nyingine tofauti, na Dunia hii ni ya watu waliotengwa tena kwa makusudi, sasa sijui tuiite "The Repulic of Biharamulo" au la! Barabara hii ilichepushwa na muheshiwa toka enzi za Mkapa na kufuatiwa na ahadi lukuki za kumalizia kipande hicho zilizotolewa Bungeni na aliyekuwa waziri mkuu enzi hizo baada ya mheshiwa huyu kubanwa na wabunge. sasa ni takribani miaka kumi na miwili na ushee tangu uongozi wa JK bado kimya!! najipa moyo kuwa hiki si kisasi kwa watu wa Biharamulo Magharibi bali ni sababu tofauti. nilidhani baada ya kupewa rungu jipya maheshiwa angetoa upendeleo wa makusudi ili kufuta dhambi hii aliyowatendelea raia wa Biharamulo lakini mmmh!
Nchi ni yetu sote na hivyo kubaguana si sawa.
 
huyu mkandarasi ameanza kazi lini wakati huko nilikuwepo june 2012 hali ilikuwa mbaya kuliko maelezo.
 
Mbona bwanga-biharamulo kuna wakandarasi kutoka china na madagasca
Upo sahihi mkuu,
Barabara ya Bwanga-Biharamulo hivi sasa inajengwa na wakandarasi wapo site tena ni wachina, nashangaa huyo aliyeanzisha thread hajatembelea eneo hilo kitambo sana.
Kwa nyongeza tu, wakandarasi pia wanaijenga barabara ya Bwanga-Runzewe kwa kiwango cha lami, na wakandarasi hivi sasa wapo site na waliojenga pembezoni mwa barabara zote mbili walishalipwa na walishahamisha makazi.

Isilalamikiwe Biharamulo ambayo ni wilaya, angelalamikia mikoa isiyo na lami kama Tabora, Kigoma, Rukwa na hii mikoa mipya ya Simiyu, Katavi etc.
 
Mkuu,

Jaribu kutembelea eneo hilo unalolalamikia ujionee kwa kinachoendelea. Ungeilalamikia barabara ya Runzewe-Bwanga ambayo nayo inajengwa na ambayo inapitia kwenye shule yake muheshimiwa iitwayo 'Magufuli High School-Boarding'...hapo ungeeleweka vema, ambapo ametelekeza barabara kuunganisha mikoa.
Magufuli mjanja bana, amepitishia lami chato ambapo gari zote hupita kwenye kituo chake kupata vyakula na mahitajio mengine, anafanya mambo kwa ramani sana.
Pia, nadhani Magufuli anataka kuwekeza eneo la Runzewe pia maana hapitishi lami hivihivi tu.
 
Unanikumbusha mbali sana, Geita, Bwanga, Runzewe,Nyakanazi, Lulenge, Kakonko.Jamani kweli kwetu ni mbali sana.Na ukitaka kusafiri unajipanga wiki nzima maana asikuambie mtu bwana
 
huyu mkandarasi ameanza kazi lini wakati huko nilikuwepo june 2012 hali ilikuwa mbaya kuliko maelezo.
Mkuu manning
June 2012 todate, ni kitambo kirefu ambacho ni miezi 11 na usheee. Tayari yapo mabadiliko eneo la wilaya hiyo, mie napita takriban kila wiki najionea.
 
Last edited by a moderator:
Upo sahihi mkuu,
Barabara ya Bwanga-Biharamulo hivi sasa inajengwa na wakandarasi wapo site tena ni wachina, nashangaa huyo aliyeanzisha thread hajatembelea eneo hilo kitambo sana.
Kwa nyongeza tu, wakandarasi pia wanaijenga barabara ya Bwanga-Runzewe kwa kiwango cha lami, na wakandarasi hivi sasa wapo site na waliojenga pembezoni mwa barabara zote mbili walishalipwa na walishahamisha makazi.

Isilalamikiwe Biharamulo ambayo ni wilaya, angelalamikia mikoa isiyo na lami kama Tabora, Kigoma, Rukwa na hii mikoa mipya ya Simiyu, Katavi etc.

Jamaa nadhani hajafika huko kitambo maana malalamiko yake ni ya miaka nane iliyopita wakati wanatengeneza barabara ya Bukoba kuunganisha na mkoa wa Mwanza kimsingi wakati barabara hiyo inajengwa barabara ambayo ilipaswa kuwekwa lami ni hiyo ya kutaka Bukoba - Muleba alafu inaunganisha kuingia Biharamulo na wakati huo hiyo njia ya kwenda Chato ilikuwa ni barabara ndogo, hivyo Magufuli alitumia akili barabara ikapita jimboni kwaake kipindi hicho Chato ilikuwa ni sehemu ya Biharamulo akijua kabisa kama ikijengwa ya Biharamulo kwa kipindi hicho hiyo inayokwenda Chato isingejengwa kutokana na vipaumbele vilivyopo kwa kipindi hicho.

Kwahiyo wengi walilalamika hatimae serikali ikabidi itafute hela na sasa inajengwa, nadhani jamaa file lake kuhusu hiyo barabara ni la long time sana, na mie nawapongeza wabunge kama Magufuli sometime japo sio poa kupendelea jimboni lakini wakati mwingine unakomaa barabara inapita jimboni kwake maana kuna wilaya zingine wabunge hajui kufanya lobbying matokeo yake lami inapita mbali ya mji makao makuu ya wilaya lami hazipiti lakini kwa wilaya ambazo zina wabunge na viongozi wa wilaya plus wananchi makini wanakomaa mpaka kinaeleweka mfano mzuri Ngara kutoka junction ya barabara kuu iendayo Rwanda ni kama 25 km lakini wakati barabara hiyo inajengwa watu wakakomaa na wilaya yao ikajengewa lami kuingia makao makuu ya wilaya, the same Tarime, lami ya kutoka Sirari imepita pembezoni mwa mji kidogo lakini ikajengwa barabara nyingine inakatiza Tarime mjini pia hata Nzega barabara imekatiza pembezoni mwa mji lakini pia ikajengwa nyingine ikakatiza katikati ya mji. Sasa kama na viongozi wengine wa mikoa including wabunge na madiwani wakati hizi barabara kuu zinajengwa wangekuwa wanapiga chapuo ni rahisi kwa maeneo yao kujengewa lami kama kuna kilometre hazizidi 30 (inakuwa rahisi kushawishi). Mfano wilaya kama Kwimba, kutoka nijiapanda (Mabuki) ya barabara kuu ya Mwanza - Shinyanga ni kilometre 27 kuingia makao makuu ya wilaya ya Kwimba ambayo ni Ngudu kama wangekumbuka kipindi zinajengwa hizi 164 km za Mwanza - Shinyanga ingekuwa rahisi kwa viongozi kuishauri serikali kuwafikiria hizo 27 km ili waunganishwe maana gharama itakuwa ndogo kama hizo kilometre zingeunganishwa kwenye tenda moja. Hata barabara ya Tabora kama viongozi wake wangekuwa makini hiyo barabara ya Nzega - Tabora ingeingizwa kwenye tenda moja wakati barabara ya Dodoma - Mwanza inajengwa huku baadae wanapigania ile ya Itigi to Tabora (wao hilo hawalioni wanashindwa kutetea maslahi ya mkoa wao matokeo yake Sumbawanga - Tunduma ambao wamekuja nyuma barabara inajengwa ). Hivyo kwa maneno mengi hayo Magufuli aliyaona hayo na sasa hivi kuna mjanja mwingine EL nae alitumia ujanja wa kuwasemea watu wa mkoa Mara kuunganishwa na mkoa wa Arusha kwa barabara ya lami huku akijua kabisa barabara itawanufaisha watu wa mkoa wa Mara lakini wakati inakwenda Arusha inapita jimboni kwake (siasa kama hizi ndio zinatakiwa wakati mwingine za kujipendelea)
 
Mkuu manning
June 2012 todate, ni kitambo kirefu ambacho ni miezi 11 na usheee. Tayari yapo mabadiliko eneo la wilaya hiyo, mie napita takriban kila wiki najionea.
Mimi nilitoka huko kipindi hicho nakubali lakini najua barabara inayojengwa ni ya Lusaunga - Biharamulo. Na ukipitia kahama -NYakanazi -Lusaunga-BIHARAMULO. Lakini-Lunazi-Katahoka -Katoke -BIHARAMULO , Bado kama imeanza naomba ushahidi , nami naambatanisha ushahidi wangu hapa SAM_3592.JPG SAM_3592.JPG SAM_3592.JPG SAM_3588.JPG SAM_3591.JPG SAM_3646.JPG
 
Back
Top Bottom