kwa muda nilioangalia nimemsikia Sugu akimpongeza kwa kujibu kama dokta na Waziri wa Serikali kwamba hakupiga mipasho kama alivyofanya Magufuli jana (nukuu yangu si neno kwa neno kama alivyosema sugu isipokua ni jinsi nilivyomuelewa)
Kwa ukweli Kigoda ameonyesha busara sana na amepokea michango hadi ya upinzani kwa roho safi. Nampongeza Sugu pia kwa kuwa mkweli na kusifia panapostahili.