Waziri Kagasheki unawaibia wananchi badala ya kuwaendeleza

  • Thread starter kakizibet mulokozi
  • Start date

K

kakizibet mulokozi

Member
Joined
Nov 26, 2013
Messages
9
Likes
0
Points
0
Age
19
K

kakizibet mulokozi

Member
Joined Nov 26, 2013
9 0 0
Tunachokielewa moja ya majukumu ya mbunge katika jimbo lolote ni kubuni fursa za kuwawezesha wapiga kura waliomchagua, inatia aibu kubwa unapomuona mbunge badala ya kubuni fursa za kuwawezesha wapiga kura wake anabuni fursa za kuwanyonya na kuwadidimiza waliomchagua, kweli ndugu wadau wa maendeleo kweli hiyo ni sahihi?

Kweli hii haina uficho wowote, kuna usemi usemao aliyenacho ataongezewa na asiyenacho hata kile kidogo atanyang'anywa kabisa, usemi huu unadhihirisha mambo yanayofanywa Katika jimbo la Bukoba mjini na waziri wa maliasili na utalii , Balozi Khamis Kagasheki, hii ni kwa kuwa fursa zote anazozibuni zinalenga kuwatesa, kuwadidimiza na kuwanyonya wananchi, imeonekana huyu bwana anatumia nafasi yake ya ubunge kufanya biashara ya kujipatia faida kubwa kupitia katika migongo ya waliomchagua.

Tusiende mbali alianzisha Chama vya akiba na mikopo ambacho hadi sasa hakina mwelekeo kabisa, hiki kimekosa mwelekeleo baada ya kuonekana ni cha kibiashara zaidi, akaanzisha mfuko mkubwa BDG alisema una lengo la kuwawezesha wananchi, ulizinduliwa na Rais wa sasa wa Zanzibar Dr Mohamed Shain, hadi sasa mfuko huo haujulikani unamnufaisha nani kwa kuwa hausikiki tena.

KInachotia aibu ni mradi wa kuwakopesha vijana pikipiki, mradi huu umegubikwa na utata kwa kuwa unadhihirisha wazi jinsi Kagasheki anavyowanyonya na kuwadidimiza wananchi, kiwaeleze katika mradi huo anayetaka kukopa pikipiki anatanguliza fedha za kiingilio shilingi 66,000 ili aweze kupata mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 1.2, kinachomuonyesha Kagasheki asivyo na mpango wa kuwaendeleza wananchi pale mkopaji anapoanza kulipa mkopo wa kipikipiki aina ya TOYO inabidi kila wiki arejeshe zaidi ya shilingi 50,000 hivyo kwa mwezi inabidi arejeshe shilingi 200,000 mkopo unaliptwa kwa kipindi cha miezi 10 hivyo katika kipindi hicho mkopaji ainabidi alipe shilingi milioni 2, mbali na hicho kiasi kuna fedha nyingine ambayo mkopaji anatakiwa kulipa zaidi ya shililingi zaidi ya 200,000, jumla yote pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.2 unakuta inamgharimu mkopaji zaidi ya shilingi milioni 2.2, kweli waziri huyo ana lengo la kuwawezesha wananchi waweze kukabiliana na umasikini wa kipato au anataka kuwanyonya watu na kuwadimiza?
 
aminangalo

aminangalo

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2013
Messages
977
Likes
3
Points
0
aminangalo

aminangalo

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2013
977 3 0
kama ni kweli hiii ni mbaya ila usikute ni uleugomvi wenu
 

Forum statistics

Threads 1,252,076
Members 481,989
Posts 29,794,766