Waziri gani bado hajatumbua jipu? Aharakishe!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Mawaziri,ili wabaki na kupendwa bila kupondwa na mamlaka,wanapaswa watumbue majipu kwenye sehemu zao. Falsafa ya hapa kazi tu ni falsafa ya tumbuatumbua baada ya kutambua.

Kwanza Waziri anapaswa kujipanga. Kutayarisha scripts. Kuandaa scene. Na ku-act kwa kutumbua kimkakati. Ili asikike na mambo yake yafike. Aonekane anawajibika kiuhakika.Sheria zitafuata,kutumbua jipu kwanza. Hakuna mchezo wala dezo liachalo uozo.

Hata yeye ameshatumbua na wamemtambua. Nauliza,Waziri gani bado hajatumbua jipu? Tafadhali aharakishe!

Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam
 
Hahahaha na kweli wana andaa scene na ku act ili waweze kuonekana na bwana mkubwa.
Ni kutumbua tu.
 
Ha
Mawaziri,ili wabaki na kupendwa bila kupondwa na mamlaka,wanapaswa watumbue majipu kwenye sehemu zao. Falsafa ya hapa kazi tu ni falsafa ya tumbuatumbua baada ya kutambua.

Kwanza Waziri anapaswa kujipanga. Kutayarisha scripts. Kuandaa scene. Na ku-act kwa kutumbua kimkakati. Ili asikike na mambo yake yafike. Aonekane anawajibika kiuhakika.Sheria zitafuata,kutumbua jipu kwanza. Hakuna mchezo wala dezo liachalo uozo.

Hata yeye ameshatumbua na wamemtambua. Nauliza,Waziri gani bado hajatumbua jipu? Tafadhali aharakishe!

Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam
Ha ha ha! hivi kumbe ni mashindano awahi fasta asije akaachwa na wenzie daaah!!
 
Nilifikiriaga kuhusu hii serikali nguvu huniishiaga sana. Hasa hasa sehemu za magotini, kidevuni, visiginoni na mdomoni......
 
Teh! Teheeeeee!!!!!!!!!

Yule mwingine ali-kitwanga badala ya kutumbua na sijui nini kilimkuta......

Mzee tupatupa wa ulevini tukumbushe wanao
 
Kutumbua nisera ambayo kila mwana CCm anaelewa nini malengo yake, kwenye Mafisadi 100 kuyapunguzia uwezo 10 haina maana kuwa Ufisadi ndio umekufa, bali ni kuuimarisha kwa stail nyengine.
 
Back
Top Bottom