Wanajamii forums, nisiwachoshe nimekutana na hili tamko la waziri afya Dr Gwajima ya kwamba ukitaka kumchapa Mtoto muombe ruhusa Kwa sababu ana haki zake.
Nikabaki najiuliza kwamba nikitaka kumwadhibu mwanangu nimuite fulani njoo, alafu Kisha nimwambie mwanangu naomba nikuchape, akikataa namwacha au sasa ndo nafanyaje? Alafu baadae viongozi mtarudi kutwambia maadili yameporoka.
======
Kauli hiyo imetolewa na Dkt. Gwajima mnamo Juni 9, 2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya Mtoto wa Afrika ambayo yataenda sambamba na uzinduzi wa Makao ya Taifa watoto katika eneo la Kikombo.
"Akili ya toto inabidi iandaliwe iweze kukubali na kukataa mafunzo ya kuficha vitendo vya ukatili. Ukimfanyia nyumbani ataenda kuvisema shuleni. Ukimfanyia nyumbani anajua kabisa kuwa mimi haifai kupigwa, kufinywa bila utaratibu. Maana ifike mahala hata kumpiga umuombe ruhusa; naomba nikuchape kidogo. Mtoto ana haki zake!"
Sasa wewe unataka kumpiga tu, unamuumiza, unamfungia ndani anaugua – atakusema. Tunakwenda kwenye Child Empowerment, yaani kum-empower mtoto tangu akiwa mdogo – kama Watoto wa mataifa mengine.
Alisema Waziri Dkt Dorothy Gwajima.