Wazee wanaiba hela za serikali siku hizi

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,198
Nimeshtuka kadri ninavyoshuhudia majipu yanavyotumbuliwa,mfano wale wazee wa BANDARI,TRA, RELI Sakata la mabehewa mabovu,leo nimeona taarifa ya habari.ITV kariakoo wanatoa risiti za analogue na electronic kibabu kinapiga hela.Hawa wazee ni ndio wanaotuimbia wimbo wa maadili na wengi wao walikuwepo kipindi cha Nyerere na kufundwa vizuri.

Ingekuwa vijana ningeelewa kuwa wanataka mali za haraka na kizazi cha sasa kimeharibika! sasa hivi vibabu na wajukuu vinaiba hela za serikali havioni kama vinatia aibu familia zao kumulikwa na TV kwa uizi!
ushauri wangu kwa wazee achieni kazi vijana.msiendelee kuaibika na majipu ya mapadlock,hana break huyu jamaa 'atamiueni' kwa presha!

Hayo tu.
 
Mwizi ni mwizi tu... na wizi ni kama ngozi... ukizoea popote utakuwa nayo..
 
Mwizi ni mwizi tu... na wizi ni kama ngozi... ukizoea popote utakuwa nayo..
kweli lakini hizo hela hataweza kula!.umri.umewatupa,ngozi zimeshajikunja na presha juu! wakipigwa miaka 10 jera sawasawa na murder case kwao.
 
Wale waliokamatwa na Masamaki kule TRA ni wazee? Wizi ni wizi tu haujali umri wa mtu!!
 
Back
Top Bottom