bottleneck
Member
- Oct 13, 2016
- 43
- 13
KARIBU MKOROMIJE SISI TUNAKUNGOJEA
Daudi bashite pole, huruma nakuonea
Koromije polepole, karibu twakungojea
ulijitia kiherehere, jiji ulilivamia
sasa unarudi na ndala, kipi ulicho sahau?
Wewe kweli ni bashite, wala usiweke vyeti
taumbuka kiokote, kichwa zero huna vyeti
ulifoji ukamatwe, haujui hisabati
Umelivamia jiji, karibu mkoromije
Cheo lipewa si haba, sasa mekufika hapa
nakitanzi mejikaba, kwa kuwataja mapapa
misifa uliibeba, sasa mbona unasepa?
Daudi mkoromije, ujitetee mwenyewe
weka magamba mezani, wacha maneno ya kanga
sigeuke hayawani, mahekaluni kutanga
sijifanye punguwani, wewe bado kifaranga
Karibu mkoromije, karibu tulime pamba
ulisomea uvuvi, njoo ziwani tuvue
sangara hata uduvi, biashara tutoboe
Umesha jipaka mavi, husafiki jiondoe
japo zero nayo namba, na chuoni ulidesa
Tamati sisemi sana, kalamu ninaitua
nakuombea kwa rabana, koromije ukitua
nafasi uliyobana, wasomi watachukua
Jipu lako li usoni, magu atalitumbua...
Daudi bashite pole, huruma nakuonea
Koromije polepole, karibu twakungojea
ulijitia kiherehere, jiji ulilivamia
sasa unarudi na ndala, kipi ulicho sahau?
Wewe kweli ni bashite, wala usiweke vyeti
taumbuka kiokote, kichwa zero huna vyeti
ulifoji ukamatwe, haujui hisabati
Umelivamia jiji, karibu mkoromije
Cheo lipewa si haba, sasa mekufika hapa
nakitanzi mejikaba, kwa kuwataja mapapa
misifa uliibeba, sasa mbona unasepa?
Daudi mkoromije, ujitetee mwenyewe
weka magamba mezani, wacha maneno ya kanga
sigeuke hayawani, mahekaluni kutanga
sijifanye punguwani, wewe bado kifaranga
Karibu mkoromije, karibu tulime pamba
ulisomea uvuvi, njoo ziwani tuvue
sangara hata uduvi, biashara tutoboe
Umesha jipaka mavi, husafiki jiondoe
japo zero nayo namba, na chuoni ulidesa
Tamati sisemi sana, kalamu ninaitua
nakuombea kwa rabana, koromije ukitua
nafasi uliyobana, wasomi watachukua
Jipu lako li usoni, magu atalitumbua...