OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 437
Zanzibar ni nchi kamili ambayo ina serikali, Baraza la wawakilishi (Bunge) pamoja na mahakama ambazo zina ushirikiano wa mambo ya kimuungano na Tanzania Bara.
Ni jambo la ajabu na fedheha kubwa kuona mtu ama kiongozi yeyote yule kuipuuzia Zanzibar na kujenga dharau kwa watu na serikali yake kwa kutumia kete ya udogo wa kijiografia ama uchache wa watu.
Kwa nyakati tofauti tofauti tumewashuhudia Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernard Membe na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakishiriki kuidharau na kuibomoa Zanzibar.
Tuanze na Bernard Membe. Membe haaminiki linapokuja suala la kuwahakikishia Wazanzibari muungano wa maridhiano, unaojali hali halisi, unaohitaji kuendeshwa kwa uwazi na ukweli, tena kwa kuzingatia kuwa watu wa nchi hizi mbili walishakuwa na mahusiano ya damu hata kabla ya hiyo 1964.
Membe anajulikana kuinyonga Zanzibar kwa kuifutia misaada ya kielimu ya Oman. Alitumia ukuu wake wa wizara anayoongoza akafuta misaada dakika chache kabla ya kusomwa tamko la kiushirikiano kati ya Tanzania na Oman alipokuja kuzuru nchini Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman, Dk. Rawiyah Al Busaid, mzaliwa wa Oman kwa baba aliyezaliwa mjini Zanzibar miaka ya 1940.
Kama hiyo haitoshi Membe alishawahi kusema Bungeni kuwa Wazanzibar wasijitutumue kwani kwake Zanzibar anauona kama ni mkoa tu. Lahaula!
Watu ambao wana serikali yao, wana Rais, wana chombo chao cha kutunga sheria (Baraza la wawakilishi), wana vyombo vya ulinzi na usalama wana mahakama utaweza kuita Zanzibar ni mkoa? Hii jeuri na dharau anayoionyesha Membe kwa Wazanzibar ameitolea wapi? Eti Zanzibar ni mkoa! Lahaula!
Kauli ambayo inataka kufanana na hiyo ilishawahi kutolewa na Waziri mkuu Mizengo Pinda ambaye yeye hakuvuka mipaka ya kuidharau Zanzibar mpaka kuita mkoa bali yeye Pinda alisema kwake Zanzibar sio nchi. Lahaula!
Membe na Pinda ambao wameonyesha dhahiri kuidharau Zanzibar ni dhahiri shahiri wanaweza kufanya mambo makubwa kwa Zanzibar endapo watapewa madaraka makubwa wanaweza kuisambaratisha Zanzibar kutoka kuwa nchi hadi kuwa mkoa, kama wanavyodai.
Ipo siku naamini endapo Membe na Pinda wakifanikiwa kuwa viongozi wakubwa watatamani kuizibia mianya yote ya kimaendeleo na fursa stahiki kwa Wazanzibar. Tuwe nao makini haswaa nyakati hizi za kumpata Rais mpya wa awamu ya tano