kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,633
- 7,021
Nilipokuwa sekondari tulisoma na wanafunzi wasioona.Siku moja ilikuwa siku ya kugawiwa ndizi(matunda) na zikagawanywa kila mtu apate angalau moja.Hata hivyo share ya wasioona ilitengwa pembeni ili wagawane wao wenyewe kwani ilihofiwa wakichanganywa na wengine wanaweza kukosa mgao wao.Kilichotokea ni kwamba baadhi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza walikosa kabisa ndizi wakati wasioona walipata ndizi tano tano!Wale wanaoona waliamua kwenda kuwaomba wasioona.Wasioona waliwanyima na walisikika wakisema"Kama sisi tusioona tumepata tano,je ninyi mnaoona si mtakuwa mmepata hata kumi?"Wazanzibar wanafaidika sana na muungano lakini kelele nyingi za kero zinatoka kwao!Watu hawa hawana shukrani na sishauri waendelee kubebwa huku wakitutapikia!
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums