Wawili wauawa na tembo shambani

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,773
2,000
Wakazi wawili wa Kijiji cha Musimi wilayani Ikungi, wamefariki dunia baada ya kushambuliwa na kundi la tembo waliovamia Kitongoji cha Italala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba alisema tukio hilo lilitokea juzi saa nne asubuhi.

Aliwataja waliouawa kuwa ni Shaaban Hassan (68) na Ayubu Emmanuel (19) na kwamba, siku ya tukio wakati Hassan akiendelea kuvuna mahindi shambani kwake kundi la tembo 32 waliingia.

“Wakati akijaribu kuwatoa shambani kwake walimvamia na kumkanyaga sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kifo chake papo hapo,” alisema.

Magiligimba alisema wakati tembo hao wakimshambulia Hassan, Emmanuel alikuwa amepanda juu ya mti ambao tembo waliuvamia naye akaachia tawi alilokuwa ameshikilia na kuanguka hivyo kupata majeraha mwilini.

“Emmanuel alipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Singida akiwa mahututi. Alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu,” alisema.

Alisema uchunguzi umebaini tembo wamekuwa wakipita kwenye kitongoji hicho kwa miaka tofauti.

Hata hivyo, Magiligimba alisema mara ya mwisho tembo walipita kwenye kitongoji hicho mwaka 1974.

Wakati huohuo, kamanda Magiligimba alisema hadi sasa thamani ya uharibifu wa mazao uliosababishwa na wanyama hao haijajulikana. Alisema wanaendelea kufanya uchunguzi zaidi juu ya uvamizi wa tembo wakishirikiana na idara ya maliasili kitengo cha wanyamapori.


Chanzo: Mwananchi
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
35,296
2,000
Mungu wapokee waja wako na uwalipe mema kadri ya matakwa yako
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom